1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yabatilisha kifungo cha mtoto wa Santos wa Angola

5 Aprili 2024

Mahakama ya Katiba ya Angola imebatilisha kifungo cha miaka mitano alichohukumiwa Jose Eduardo dos Santos, mtoto wa rais wa zamani kutokana na makosa ya utakatishaji fedha.

https://p.dw.com/p/4eSHl
Angola Jose Eduardo dos Santos na Joao Lourenco
Marehemu Jose Eduardo dos Santos (kushoto) na mrithi wake wa urais wa Angola, Joao Lourenco.Picha: Marco Longari/AFP

Majaji wa mahakama hiyo ya juu katika mji mkuu wa Luanda walitangaza siku ya Alkhamis (Aprili 4) kwamba hukumu iliyotolewa mwaka 2020 dhidi ya Jose Filomeno dos Santos ilikuwa batili na "kinyume cha katiba".

Filomeno dos Santos, mwenye umri wa miaka 46, amekuwa akitumikia hukumu yake kwa kifungo cha nyumbani baada ya kutiwa hatiani kwa kuiba dola milioni 500 kutoka hazina ya serikali ambayo aliisimamia kuanzia 2013 hadi 2018.

Soma zaidi: Binti wa rais wa zamani wa Angola anakanusha madai ya ufisadi

Hata hivyo haijabainika iwapo mtoto huyo wa marehemu Eduardo dos Santos aliyepewa jina la utani "Zenu" ataachiwa  huru au atafunguliwa kesi mpya.

Zenu alikuwa mtu wa kwanza kwenye familia ya rais wa zamani kufunguliwa mashtaka kama sehemu ya kampeni ya kupinga ufisadi iliyoongozwa na Rais Joao Lourenco tangu alipoingia madarakani mnamo 2017.