1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeshi yapambana na waandamanaji Misri

5 Mei 2012

Majeshi ya Misri yamewashambulia waandamanaji kwa mabomba ya maji,mabomu ya kutoa machozi pamoja na risasi ,wakijaribu kuwazuwia kufanya maandamano kuelekea katika jengo la wizara ya ulinzi siku ya Ijumaa.

https://p.dw.com/p/14qOU
Egyptian soldiers raise their batons at a protester during clashes outside the Ministry of Defense in Cairo, Egypt, Friday, May 4, 2012. Egyptian armed forces and protesters clashed in Cairo on Friday, with troops firing water cannons and tear gas at demonstrators who threw stones as they tried to march on the Defense Ministry, a flashpoint for a new cycle of violence only weeks ahead of presidential elections. (Foto:Ahmed Gomaa/AP/dapd)
Wanajeshi wakipambana na waandamanajiPicha: dapd

Mapambano  hayo  makali  ya  mitaani  yameongeza  hali ya  wasi  wasi  ya  kuzuka  kwa  wimbi  jingine  la  ghasia kuelekea  katika  uchaguzi  ujao  ambao  ni  wa kumchagua  rais  mpya  ambaye  atachukua  nafasi  ya rais  aliyeondolewa madarakani  mwaka  mmoja  uliopita Hosni  Mubarak.

Kwa  mara  ya  kwanza katika  kipindi  cha  mpito  nchini Misri  ambacho  kimeambatana  na  ghasia , Waislamu wenye  imani  kali , badala  ya makundi  ambayo  hayafuati imani  za  kidini , wamekuwa  mstari  wa  mbele   katika mapambano   dhidi  ya  watawala  wa  kijeshi  ambao wamekuwa  wakishutumiwa  kwa  kujaribu  kung'ang'ania madarakani.

Egyptian security forces, unseen, fire a water cannon at protesters during clashes outside the Ministry of Defense in Cairo, Egypt, Friday, May 4, 2012. Egyptian armed forces and protesters clashed in Cairo on Friday, with troops firing water cannons and tear gas at demonstrators who threw stones as they tried to march on the Defense Ministry, a flashpoint for a new cycle of violence only weeks ahead of presidential elections. (Foto:Ahmed Gomaa/AP/dapd)
Wanajeshi wakitumia maji kuwatawanya waandamanajiPicha: dapd

Marufuku  kulikaribia  jengo la wizara ya ulinzi

Baraza  la  kijeshi  limeweka amri  ya  kutotembea kuanzia mchana  hadi  alfajiri  katika  eneo  linalozunguka  wizara ya   ulinzi, ambalo  limekuwa  sehemu  ya  mapambano kwa  waandamanaji  wenye  hasira  baada  ya  watu  tisa kuuwawa  siku  ya  jumatano, ambapo  wengi  wao walikuwa  ni  waungaji  mkono  wa  mgombea  ambaye ameenguliwa  kutoka  kundi  la  Waislamu  wenye msimamo  mkali.

Ghasia  hizo  zimeiweka  kampeni  ya  uchaguzi  wa  hapo Mei  23 hadi 24  katika  mtafaruku  mkubwa, wakati wagombea  wawili  wanaoongoza   pamoja  na  wagombea wengine  kadha  wakiahirisha  kwa  muda  kampeni  zao wakipinga  hatua  za  jeshi  kushughulikia  hali  hiyo.

Egyptian protestors run for cover from tear gas fired by security forces during clashes near the Interior Ministry in Cairo, Egypt, Saturday, Feb. 4, 2012. The number of people killed in clashes with Egyptian security forces in the wake of a deadly soccer riot rose on Saturday, according to a field doctor and a security official, as demonstrators in Cairo kept up their calls for an end to military rule and retribution for those killed in the soccer game violence. (Foto:Khalil Hamra/AP/dapd)
Hali si shwari mjini CairoPicha: dapd

Waandamanaji wakusanyika tena Tahrir

Maelfu  ya  waandamanaji  walikusanyika  katika  eneo  la Tahrir  mjini  Cairo , sehemu  ambayo imetumika  katika vuguvugu  la  mapinduzi  ya  umma  mwaka  jana. Waandamanaji  walikuwa  ni  pamoja  na  waungaji  mkono wa  kundi  la udugu  wa  Kiislamu  na  Waislamu  wa madhehebu ya  Salafi, lakini  pia  vijana  wanamapinduzi ambao  waliongoza  maandamano  ya  umma  ambayo yalimuondoa  madarakani  rais  Hosni  Mubarak  walishiriki.

Licha  ya onyo  kutoka  kwa  maafisa  wa  serikali  dhidi  ya kukusanyika, makundi  hayo  yaliandamana  hadi  katika wilaya   ya  Abbasiyah  na  kujiunga  na  hatua  ya  kukaa chini  nje  ya  jengo  la  wizara  ya   ulinzi , ambalo  hapo kabla  lilikuwa  limeshikiliwa  na  waungaji  mkono  wa mgombea  uchaguzi  wa  kundi  la  Kiislamu  Hazem Abu Islami.

Mwanasheria  ambaye  amegeuka  kuwa   mhubiri  wa  dini, Abu Ismail  mfuasi  wa   imani  kali  ya  kidini  alienguliwa kutoka  katika  kinyang'anyiro  cha  urais kwasababu marehemu  mama  yake anadaiwa  aliwahi  kuwa  na  uraia wa  nchi  mbili Misri  na  Marekani , na  kumfanya kutokubalika  kisheria  kushiriki  katika  kinyang'anyiro hicho  cha  urais  chini  ya  sheria  za  uchaguzi. Amewahamasisha  wafuasi  wake  kuingia  mitaani . Tunakabiliwa  na  njama  za  kuharibu mapinduzi, amesema  msemaji  wake  Gamal Saber  alipozungumza na  shirika  la  utangazaji  la  Al-Jazeera.

Mwandishi: Sekione Kitojo /ape

Mhariri : Stumai George