1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makamo wa rais wa Marekani ziarani Mashariki ya kati

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2i

Riyadh:

Makamo wa rais wa Marekani Dick Cheney yuko njiani kuelekea Saud Arabia kusaka msaada kwaajili ya Irak.Miezi miwili iliyopita Mfalme Abdallah, alikosoa vikali kile alichokiita “kukaliwa Irak na wageni kinyume na sheria ”.Makamo wa rais wa Marekani Dick Cheney anatazamiwa pia kuzitembelea Misri na Jordan mwishoni mwa wiki hii.Lengo la ziara hii ya wiki moja ya Dick Cheney ni kuwasihi marafiki wa Marekani katika mashariki ya kati wakubali kuwashawishi wasunni washiriki katika utaratibu wa kisiasa nchini Irak.Ziara yake hiyo imelengwa pia kusaka uungaji mkono wa waarabu katika kupunguza ushawishi wa Iran .Makamo wa rais wa Marekani alionya hapo jana,nchi yake itashirikiana na “wengine” ili kuzuwia Iran isimiliki silaha za kinuklea na kulidhibiti eneo hilo.