1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makombora ya Urusi yauwa watu watano Ukraine

Sudi Mnette
2 Mei 2024

Watu watano wameuawa baada ya Urusi kufanya mashambulizi katika maeneo ya mashariki mwa Ukraine ya Kharkiv na Donetsk. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa mamlaka katika maeno hayo.

https://p.dw.com/p/4fP9L
Russland Krieg Ukraine
Mwili wa mtu aliyeuawa katika shambulio la anga la Urusi unaonekana kwenye gari lake Zolochiv, mkoa wa Kharkiv, Ukraine, Jumatano, Mei.1Picha: Andrii Marienko/AP/picture alliance

Gavana wa eneo la Kharkiv, Oleg Synegubov amesema katika eneo hilo lenye kupakana na Urusi, bomu liliwauwa watu wawili na wengine sita wakijeruhiwa akiwemo mtoto wa umri wa miaka 11.

Pamoja na ripoti za visa vya mauwaji mengine katika eneo la upande wa mashariki zaidi katika mkoa wa Kharkiv karibu na mji wa Kupiansk, makombora ya Urusi yamemuua mwanamke wa umri wa miaka 67 katika kijiji cha Lelyukivka.

Eneo hilo ambalo sehemu kubwa zinadhibitiwa na vikosi vya Urusi kwa miezi kadhaa baada ya kuvamia Februari 2022, linakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya Urusi.