1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Mamia ya watu wafanya maandamano nchini Tunisia

Tatu Karema
12 Mei 2024

Mamia ya waandamanaji walikusanyika mjini Tunis, Tunisia kutaka kuachiliwa huru kwa waandishi wa habari, wanaharakati na viongozi wa upinzani waliofungwa, na pia kupangwa kwa tarehe ya uchaguzi wa rais ulio wa haki

https://p.dw.com/p/4flDE
Maandamano yalioongozwa na chama cha Ennahda nchini Tunisia dhidi ya Rais Kais Saeid mnamo Julai 26, 2021
Maandamano yalioongozwa na chama cha Ennahda nchini TunisiaPicha: Chedly Ben Ibrahim/NurPhoto/imago images

Imed Khemiri, afisa mwandamizi katika chama cha Ennahda ambacho ni mshirika wa chama cha Salvation Front kinachoandaa maandamano hayo, amesema kuwa kwa sasa hakuna mazingira ya uchaguzi wa haki na pia hakuna tarehe iliyopangwa ya kufanyika kwa uchaguzi huo huku mamlaka ikiwakandamiza wanasiasa, wanasheria na waandishi habari.

Changamoto zinazoikabili Tunisia

Maandamano hayo yanakuja huku kukiwa na mzozo wakiuchumi na kisiasa na wimbi la kukamatwa kwa wanahabari, wanasheria, wanaharakati na wapinzani nchini humo.

Hapo jana, polisi nchini humo walivamia jengo la mawakili na kumkamata Sonia Dahmani, wakili anayejulikana kwa ukosoaji wake mkali wa Rais Kais Saied. Waandishi wawili wa habari pia walikamatwa siku hiyo hiyo.