1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man City wabeba Kombe la Dunia la Vilabu

Bruce Amani
23 Desemba 2023

Manchester City imeshinda Kombe la Dunia la Vilabu kwa mara ya kwanza na kuhitimisha mwaka wa 2023 na mataji matano. City wamewacharaza Fluminense 4 - 0 mjini Jeddah Ijumaa usiku.

https://p.dw.com/p/4aWI7
Fußball Saudi Arabien | Club WM |  Manchester City v Fluminense
Manchester City sasa wamebeba makombe matano katika mwaka wa 2023Picha: GIUSEPPE CACACE/AFP

Manchester City imeshinda Kombe la Dunia la Vilabu kwa mara ya kwanza na kuhitimisha mwaka wa 2023 na mataji matano. City wamewacharaza Fluminense 4 - 0 mjini Jeddah Ijumaa usiku. 

Soma pia: Manchester City hatimaye ni mabingwa wa Ulaya

Ushindi wa City umeendeleza utawala wa vilabu vya Ulaya kwenye mashindano hayo tangu mwaka wa 2012. Vilabu vya Ulaya vimeshinda mechi 22 mfululizo katika mashindano ya Kombe la Dunia la Vilabu.

Julian Alvarez aliifungia City bao la ufunguzi katika sekunde ya 45 kabla ya mchezaji wa Fluminense Nino kujifunga katika kipindi cha kwanza.

Phil Foden na Alvarez waligongelea msumari wa mwisho baadae katika kipindi cha pili. Baada ya kutwaa Champions League kwa mara ya kwanza na klabu hiyo, Premier League na Kombe la FA msimu uliopita, City pia walibeba UEFA Super Cup kwa mara ya kwanza mwezi Agosti.