1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manchester United yaipiga kumbo AC Milan 4:0

11 Machi 2010

Leo ni zamu ya Kombe la Ligi la Ulaya

https://p.dw.com/p/MPbo
Manchester United ikimshangiria Rooney kwa mabao yake.Picha: AP

Baada ya Manchester United ukiichezesha jana AC Milan ya Itali "kindumbwe-ndumbwe charia " na kuifedhehi uwanjani old Traford na Olympique Lyon ya Ufaransa, kuwapiga kumbo nje ya champions League- mabingwa mara kadhaa wa ulaya na mastadi wao akina Cristiano Ronaldo na Kaka, jioni hii klöabu 3 za Ujerumani zimevuinjari nazo kufuzu kwa robo-finali ya Kombe jengine la la ulaya-Euro-League.

Miongoni mwa changamoto za jioni hii,Werder Bremen iliocheza finali ya mwaka jana ya Kombe la UEFA la Ulaya,imefunga safari hadi Valencia,Spain.Valencia, iko nafasi ya 3 ya ngazi ya Ligi ya Spain na inakumbuka darasa iliofunzwa na Bremen pale timu hizio mbili zilipokutana 2004 katika kinyan'ganyiro cha champions League.

Bremen ilitamba kwa mabao 2-1 nyumbani na mabao 2:0 huko Valencia. Valencia,inadai "mla, ni mla leo, mla jana kala nini ?" Na ikicheza nyumbani,Valencia imejiwinda kulipiza kisasi cha mwaka 2004.Wolfsburg , mabingwa wa Ujerumani wana miadi na Rubin Kasan ya Urusi.

Hamburg,pia ya Ujerumani na mabingwa wa kombe hili la ulaya ,1983, ilipotamba na muingereza Kevin keegan, ina miadi leo na Anderlecht ya Ubelgiji.Hamburg iliilaza Anderlecht katika finali ya Kombe la washindi la ulaya (Winners cup) 1967 na kutoroka na Kombe.Na kwavile, "mramba asali, harambi mara moja",Hamburg inataka kuonja tena asali jioni hii.

Wasi wasi wa Hamburg leo, ni beki wao mshahara Jerome Boeteng ambae haijulikani iwapo ni fit kucheza leo.Kwa kila hali, Hamburg itakata kusonga mbele na kucheza finali ya Kombe hili iliopangwa nyumbani mwao Hamburg hapo Mei 12.Liverpool ya Uingereza ina pambana na Lille ya Ufaransa wakati Fulham wana kibarua kigumu kuzima vishindo vya wataliana-Juventus.

Jana, ilikua tena siku ya Wayne Rooney, katika changamoto ya Kombe la champions League.Rooney ,alilifumania lango la AC Milan ya Itali, mara mbili kabla Manu kuizika kabisa Milan katika kaburini Old Traford kwa mabao 4:0.

AC Milan bila ya mlinzi wao mashuhuri Alessandro Nesta,mshambulizi hatari Alexandre Pato na stadi wa kiungo Luca Antonini, walikwenda kapa.Kwani Manu waliwavamia kuanzia dakika ya mwanzo hadi ya mwisho.Hata kuingia uwanjani kwa stadi wa zamani wa Manu, David Beckham, uüpande wa Milan, hakukusaidia kitu.Mkwaju wa Beckham mkali na maridadi ajabu katika lango la Manu ,uliokolewa.

Mkono wa buriani kuaga kombe hili la champions League, msimu huu,haukwenda tu kwa AC Milan ya Itali hapo jana ,bali hata kwa wenzao Real Madrid,timu ilioweka rekodi kwa kutwaa kombe hili la klabu bingwa barani ulaya si chini ya mara 9.

Kwa mara ya 6 Real Madrid ,licha ya kutumia vitita vikubwa vya fedha kuwanunua akina Kaka wa Brazil na Cristiano Ronaldo wa Ureno, "waliula na chua kwa uvivu wa kuchagua." kwani, baada ya jana Ronaldo kulifumania lango la Lyon na mapema, Real ,ilifanya uzembe kuongeza mabao na kufuta madhambi waliofanya huko Ufaransa walipozabwa bao 1:0 na Lyon. Pale, Lyon ,iliposawazisha bao la Ronaldo, Real haikuamini macho yake na vishindo vyao vya kuongeza bao la pili na la ushindi, vikuwa vya darini tu, vilivyoishia sakafuni.Mwishoe, klabu 2 zilizonyakua Kombe hili kuliko nyengine zozote, Real na M ilan, zkaga champions league alao kwa msimu huu.

Mwandishi: Ramadhan Ali /DPAE

Imepitiwa na :Hamidou Oummilkheir