1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: 2016 mwaka wa kutisha kwa mara nyingine

27 Desemba 2016

Wajerumani wengi wanaiangalia hali yao binafsi kuwa nzuri, ila ukweli hauko hivyo. Kwasababu muonekano wa siasa za dunia, unaelekea katika matatizo makubwa. Ni maoni ya mhariri mkuu wa DW Alexander Kudascheff.

https://p.dw.com/p/2Uu28
Symbolbild Deutschland Europa Flagge
Picha: picture-alliance/dpa

Mwaka 2016 pia ulikuwa mwaka wa kutisha. Dunia imetumbukia katika hali ya mparaganyiko. Katika mashariki ya kati vita vinaendelea - nchini  Syria , Yemen , Libya na  pia  Iraq. Kundi linalojiita  Dola  la  Kiislamu , linalofanya  unyama  wa  kuogofya, mauaji, ugaidi  wa  itikadi  kali, bado  haujamalizwa. Hali  tete  ya vuguvugu  la  mapinduzi  ya  mataifa  ya  kiarabu  ndiyo  yaliyozusha hali  hii , kupitia ukandamizaji , matumizi  ya  mabavu, na  udikteta. Na kutokana  na  athari  hizo  na  kitovu  cha  tetemeko  hilo  kutoka katika  eneo  hilo, huenda  ikatikisa  siasa  za  dunia  pamoja  na kuzusha  mripuko  wa  kijamii, ama  hata pengine  tayari  umezusha hali  hiyo.

Inaonekana  kwamba  eneo  hilo  la  mashariki  ya  kati  limetumbukia katika vita miaka 30 iliyopita, ambapo  koo, kabila  na  jamii  za  kidini ni  mambo  ambayo  yanasababisha  mapambano.

Katika  pwani  za  mataifa ya bara  lote la Ulaya waliwasili  wakimbizi kutoka  mataifa  ya  Mashariki  ya  Kati  na  kusababisha  mshituko na  mtikisiko. Mzozo  wa  wakimbizi  tayari  umeweka  wazi, kwamba suala  la  "mshikamano  wa  mataifa  ya  Ulaya " ni  neno  ambalo limeingia  kiwingu .

Kudascheff Alexander Kommentarbild App
Mhariri mkuu wa DW Alexander Kudascheff

Brexit , neno  linalotumika  kwa  kujitoa  kwa  Uingereza  katika Umoja  wa  Ulaya , limeiingiza  jamii  ya  Ulaya  katika  mashaka makubwa.  Kazi  ya  pamoja  ya  kutafuta  amani  iliingia  majaribuni , na  jamii ilielekeza   njia  ya  kuchukua  katika  mustakabali  wa  nchi yao.

Kwa  sasa  ni  hakika  , kwamba  pamoja  na  Ulaya  Mashariki kurejea  katika  hali  ya  mataifa  kujiamulia  mambo  yao  wenyewe na  kuwa  na  utambulisho  wake,  katika  miaka  ijayo  pia  mataifa ya  Ulaya  Magharibi  yanaonekana  kuwa  yatabadilisha  utendaji wa  madaraka. Nchini  Uholanzi  inaonekana  kupitia  Geert Wilders na  nchini  Ufaransa  pia  bila  shaka  kutakuwa  na  rais  mpya , huenda  ni Mkatoliki, "mfuasi  wa  siasa  za  Thacher", ni mapinduzi ya  aina  gani  yatakayotokea.

Na  hata  nchini  Ujerumani , nchi  ambayo  ilionekana  kuwa  mhimili wa  uthabiti , kutakuwa  na  uchaguzi  mwezi  Septemba. Hakuna  mtu kwa  hivi  sasa  anayeweza  kufikiria , kwamba  Angela  Merkel, atakuwa  na   muungano  gani , ama  kwamba  atabaki  katika wadhifa  wa  Ukansela.

Ni ngome  kuu  ya  siasa  za ndani  na  nje  duniani ,  na  hii  ni kwa miaka  takriban 11  iliyopita. Lakini  hata  hapa  nchini  chama  cha siasa  kali  za  mrengo  wa  kulia  cha  Altenative  for Germany AfD, kimeingia  katika  bunge  la  taifa  na  kinaonekana  kupata  uungwaji mkono  mkubwa. Hapa Ujerumani pia watashinda  wale  wenye mawazo  ya siasa  kali  za  mrengo  wa kulia, hata  kama hawataweza  kuchukua  madaraka  ya  nchi.

Ujerumani  itaendelea  kuwa  na  uongozi  imara. Na  ndio  sababu Ujerumani itaendelea  kuwa  sehemu  ya  utulivu  katika  siasa  za dunia  ambazo  hazina  utulivu na  za  wasi  wasi. Na  hii  ni  licha  ya shambulizi  ya  kigaidi  la mjini  Berlin  muda  mfupi  kabla  ya  sikukuu ya  Krismasi, shambulio  ambalo  liliitikisa  nchi  hii  kwa  kiasi kikubwa.

Mwandishi: Alexander Kudascheff . /ZR /  Sekione  Kitojo

Mhariri : Yusra Buwayhid