1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Kombe la Dunia 2014

10 Juni 2014

Fainali za kombe la dunia zinakaribia kuanza nchini Brazil, Juni 12, Brazil inakwaana na Croatia katika mchezo wa ufunguzi. Wasikilize wataalamu wa michezo wakijadiliana kuhusu tamasha hilo.

https://p.dw.com/p/1CEy2
Brasilien Fußball WM 2014 WM-Ball Brazuca
Picha: adidas/picture-alliance/dpa

Je, ni timu gani itakayotamba mara hii katika fainali hizi? Timu gani ya Afrika inaweza kuvuka kiwango cha robo fainali na kuwa timu ya kwanza kutoka bara hilo kuingia katika nusu fainali ya mashindano haya makubwa ya soka duniani. Je, Uhispania itatamba tena na mtindo wake wa tiki taka? Na Timu za bara la Ulaya zitavunja mwiko wa kutolinyakua kombe hilo katika ardhi ya America ya kusini? Hayo na mengine mengi yanajadiliwa katika kipindi cha maoni. Wanaoshiriki ni pamoja na Ramadhan Ali mhariri wa zamani wa dawati la michezo la DW, Mtemi Ramadhani mchezaji wa zamani wa timu ya Simba na Taifa Stars, ambaye ni mshauri wa habari za michezo wa gazeti la Spoti Starehe mjini Dar Es Salaam, Fatma Likwata mtangazaji wa habari za michezo wa Cluods FM mjini Dar Es Salaam na Stephen Mukangai wa kituo cha televisheni ya KTN Nairobi Kenya. Mwenyekiti ni Sekione Kitojo.

Kusikiliza makala haya tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.