1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Mashambulizi yasiyokuwa na athari ila yana ujumbe

Caro Robi
14 Aprili 2018

Habari njema kwanza: Vita vya tatu vikuu havijaanza. Habari mbaya, mashambulizi ya anga nchini Syria hayajaleta unafuu kulingana na maoni ya mwandishi wa DW Christian F. Trippe.

https://p.dw.com/p/2w3bd
Quadriga 22.03.2018 -  Trippe, Christian
Picha: DW

Ulimwengu ulikuwa karibu kwa kiasi gani kushuhudia vita kati ya nchi mbili zenye nguvu kubwa za kinyuklia, Marekani na Urusi, katikati ya mwezi Aprili mwaka 2018? Huenda hayo tukayajua tu pengine baada ya muda.

Kwa sasa kinachoonekana wazi ni kuwa Marekani, Uingereza na Ufaransa zilijizuia, zikilenga mashambulizi yao ya kijeshi katika maeneo ambayo yanahusishwa na utengenezaji na uhifadhi wa silaha za sumu Syria.

Idadi ya raia walioathiriwa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa Jumamosi Syria kufikia sasa na baada ya tathmini ya yaliyojiri ni kama kimsingi hakuna walioathirika.

Ufanisi mpya wa Jeshi?

Katika siku za hivi karibuni, mashambulizi ya makombora yaliyofanywa Syria yamelinganisha na mzozo wa makombora uliofanyika Cuba katika kipindi cha nyuma kati ya muungano wa kisovieti na Marekani mwaka 1962.

Kinaya ni kuwa ulimwengu wakati huo na hivi sasa uko katika hali ya kushuhudia maamuzi mazito yanayochukuliwa na Rais wa Marekani, Donald Trump, wakati ambapo maafisa wa Urusi wakionya kutakuwa na athari.

Lakini wakati huo wa mzozo wa Cuba lilikuwa ni suala la kudumisha uthabiti wa kisiasa wa pande zote dhidi ya majenerali na "Dakta Seltsams"- tashtiti ya kisiasa inayoelezea hofu ya mzozo wa nyuklia wakati wa vita baridi. Hayo yalifanikiwa miaka 56 iliyopita. Mzozo unasalia kuwa wa kisiasa.

Lakini sasa, siku chache kabla ya mashambulizi ya angani Syria maonyo yalitolewa kutoka kila pande, ambapo wakati mwingine yalisikika kama sauti za majonzi.

Matumaini ni kuwa wakati huu jeshi litachukua maamuzi yapasayo. Ufanisi, na uzoefu wa majenarali wa kijeshi dhidi ya kutegemea wanasiasa wasio na ufahamu, mtu anahitaji kuwa na uwezo wa kuona kichekesho cha kisiasa ili kuona kuwa kutakuwa na manufaa katika hali hii.

Maamuzi makini ya malengo

Kukumbusha tena, kuna maelfu ya wanajeshi wa Urusi nchini Syria wanaomuunga mkono Rais Bashar al Assad. Tayari miezi miwili iliyopita, mamluki wa Urusi waliuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la angani la Marekani kaskazini mwa Syria.

Mzozo haukutokea. Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani unaopambana dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali wa kundi la Dola la Kiislamu wanafanya operesheni kaskazini mwa Syria. Kipindi hiki mashambulizi ya angani yalipangwa kwa njia ambayo hakuna wanajeshi wa Urusi walilengwa.

Mawasiliano kati ya viongozi wa kijeshi wa Marekani na maafisa wakuu wa jeshi la Urusi yanaonekana kuwa thabiti. Wataalamu wanaripoti kuwa kwa muda mrefu kuaminiana na kujiendesha kwa kitaalamu kati ya majeshi ya pande hizo mbili hakujaathirika licha ya kuwepo mvutano mpya kati ya Mashariki na Magahribi.

Syria huenda ikachukulika kuwa eneo la vita lisilotabirika katika historia. Mara kwa mara kuna majeshi yanayokabiliana ambayo nchi zao aidha zinashirikiana au ni mahasimu wakubwa kisiasa.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria vimeamuliwa na Urusi kuingilia kati kuunga mkono utawala wa Assad na pia Iran kuunga mkono. Mashambulizi yaliyofanywa na nchi tatu za magharibi zenye nguvu hazibadilishi hilo. Sio kwamba hatua zilizochukuliwa na nchi hizo hazina maana.

Mashambulizi hayo ya angani ya ujumbe

Marekani, Uingereza na Ufaransa zimeweka mambo mawili bayana na mashambulizi ya angani waliyofanya: Matumzi ya silaha za sumu za maangamizi makubwa zilizopigwa marufuku hayawezi kukosa kuwa na athari na kukanusha na kufunika uhalifu wa kivita hauwezi kuvumilika.

Mbali na hayo, nchi za magharibi zenye nguvu hazitaki kusafisha mizozo iliyotokana na siasa za kikanda hata baada ya miaka ya kupotoshwa, siasa chafu ndiyo chanzo cha mizozo hiyo.

Kanda ya Mashariki ya Kati inakabiliwa na mkondo mpya ambao haupaswi kufanyika na Urusi na Iran pekee. Huu ndiyo ujumbe wa nchi mbili - wa mashambulizi yaliyolenga viwanda vya Assad.

Na tatu, Marekani haichukui hatua peke yake bali kwa ushirikiano na Ufaransa na Uingereza, muungano wa kijeshi, lakini pia kwa makabuluano ya ushirikiano wa karibu wa kisiasa. Katika mwaka wa pili wa utawala wa rais Donald Trump, pengine hizi ni habari njema Jumamosi hii.

Mwandishi:Trippe, Christian F.

Tafsiri: Caro Robi

Mhariri: Josephat Charo