1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Mwisho wa matumaini ya uwongo Myanmar

2 Februari 2021

Jeshi la Myanmar limefanya mapinduzi na kumkamata kiongozi wa kiraia Aung San Suu Kyi. Mwandishi wa DW Rodion Ebbighausen katika maoni yake anasema ni dhahiri majaribio ya mfumo wa kidemokrasia yameshindikana

https://p.dw.com/p/3ohtn
Myanmar Militärputsch
Picha: AFP via Getty Images

Wakati jeshi la Myanmar lilipoanza kujiondowa katika siasa za kiraia mnamo mwaka 2011 moja ya swali kubwa kabisa lilikuwa ni je ni mamlaka kiasi gani jeshi hilo liko tayari kuyaachia. Waliokuwa na mashaka kuhusu suala hilo hawakuwa na imani na majenerali na walichokuwa wakikiona ni udikteta ulioendeshwa na jeshi waliojificha chini ya kivuli cha Demokrasia. Hata hivyo waliokuwa na matumaini waliiangalia kama ni hatua ya kweli ya mwanzo mpya na nafasi ya kuleta demokrasia nchini humo.

Soma pia: Baraza la usalama kujadili mapinduzi ya Myanmar

Huko mwanzo dalili nzuri zilishuhudiwa nchini Myanmar, Jeshi likiongozwa wakati huo na aliyekuwa jenerali na rais aliyeunga mkono mageuzi alikuwa na nia ya dhati kuhusu kuleta uwazi nchini humo. Aung San Suu Kyi aliachiwa huru kutoka kifungo cha nyumbani alichokuwa amewekewa,kadhalika wafungwa wengine wengi wa kisiasa wa chama chake cha National League for Democracy NLD. Kwa upande mwingine sheria kali zilizokuwepo dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari pia zikalegezwa.

Na baada ya chama hicho kikuu cha kisiasa cha NLD kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa bunge wa mwaka 2015 jeshi na chama chao cha Union Solidarity and Development walikubali kushindwa. Katika suala hilo hapakuwa na kitisho kikubwa kilichojitokeza kwenye hatua hiyo.Na kumbuka kwamba kwa mujibu wa katiba nchini Myanmar jeshi linashikilia robo ya viti vya bunge sambamba na wizara za ulinzi, usalama wa mipaka na mambo ya ndani.

Thailand Anhänger aus Myanmar protestieren für Aung San Suu Kyi
Suu Kyi amewekwa kizuizini pamoja na viongozi wenginePicha: Sakchai Lalit/AP/picture alliance

Lakini pamoja na hayo zilionekana dalili wakati huo kwamba jeshi lilikuwa tayari kuwa na maelewano au mwafaka. Chama cha NLD kilifanikiwa kupitia ushindi huo wa 2015 kulipiku jeshi na kumfanya Aung San Su Kyi mshauri mkuu wa serikali cheo ambacho ni sawa na waziri mkuu wa nchi ,na ambacho hakipo kikatiba.

Soma pia: Ulaya yaungana dhidi ya mapinduzi ya kijeshi Myanmar

Mpangaji mkuu wa mchakato mzima huu ni wakili akiitwa Ko Ni na alikuwa mkosoaji mkubwa wa jeshi la Mnyanmar,alipigwa risasi na kuuwawa barabarani mbele ya uwanja wa ndege wa mjini Yangon mara tu baada ya hatua hiyo. Waliohusika walikamatwa lakini viranja waliokuwa nyuma ya shambulio hili hawakuwahi kutambuliwa hadi leo.

Lakini iilionesha kana kwamba jeshi lilikuwa likituma ujumbe kwa chama cha NLD,kwamba msitujaribu,msipambane na sisi. Jeshi ambalo linajiona kama ndio nguzo ya uthabiti na mshikamano wa taifa hilo halikutaka kukubali kwamba mtu mwingine atabeba jukumu la kuamua mwelekeo wa taifa.

Hata hivyo chama hicho cha NLD kiliendelea kuelekeza nguvu zake katika makabiliano,kuliko kushughulikia suala la mageuzi ambayo yangesaidia kuwapa manufaa wananchi,chama hicho badala yake kilielekeza nguvu kubwa katika ahadi ya mageuzi ya katiba ambayo haikutelekelezwa kutokana na jeshi kuweka vizuizi.

Myanmar Militärputsch | Myint Swe, acting president
Kaimu rais wa Mnyanmar Myint SwePicha: MRTV/Handout/REUTERS

Uhusiano kati ya Suu Kyi na mkuu wa majeshi Min Aung Hlaing ulianza kuwa mbaya na kuonekana waziwazi.Na wala kitendo cha mwanasiasa huyo cha kusimama katika mahakama ya haki ya kimataifa ICJ mjini The Hague alikoitetea nchi yake na jeshi dhidi ya tuhuma ya kuendesha mauaji ya halaiki dhidi ya jamii ya Warohingya hakikuubadili ukweli huo wa kuwepo hali mbaya ya uhusiano na jeshi.

Soma pia: Dunia yalaani mapinduzi ya kijeshi Myanmar

Na uchaguzi ndio ulionekana unaweza kuwa njia ya mwisho ya kuibadili hali hiyo lakini ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Novemba 2020 wa San Suu Kyi na chama chake wa asilimia 83 haukulifurahisha jeshi. Na mara hii jeshi hilo liliyapinga matokeo na kudai mizengwe ilifanyika. Tume huru ya uchaguzi iliyowekwa na serikali ya kiraia ilizipinga tuhuma za jeshi. Lakini jeshi lilikwenda mbali na kufungua kesi kwenye mahakama ya juu ambayo bado haijatowa uamuzi.

Soma pia: Myanamar: Jeshi limetangaza hali ya dharura na kuchukua madaraka

Sasa jeshi limeamua kufanya mapinduzi na linataka kuchukua mamlaka ya kuiongoza serikali kwa mwaka mmoja ili kuleta mageuzi ikiwemo mageuzi ya tume ya uchaguzi. Kifungu nambari 417 cha katiba kinahalalisha mapinduzi na kuliruhusu jeshi kuchukua madaraka ikiwa hali ya dharura inatishia uhuru au mshikamano wa nchi. Kwa maana hiyo jeshi linajiona liko sahihi.Kwa mantiki hii mapinduzi nchini Myanmar yanaliongezea nguvu jeshi uhalali wa kuivunja Demokrasia ili kwa uapnde mwingine kuinusuru Demokrasia hiyo hiyo. Sasa suali ni je ni mamlaka kiasi gani hatimae jeshi liko tayari kuyaachia?Jibu liko wazi,jeshi haliko tayari kuachia mamlaka.

https://www.dw.com/en/opinion-no-more-illusions-in-myanmar/a-56409670