1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahariri wanazungumzia kuhusu bajeti ya Ujerumani iliyopitishwa bungeni ...

Kitojo, Sekione3 Julai 2008
https://p.dw.com/p/EVb4


►◄


Wahariri  wa  magazeti  ya  Ujerumani  hii  leo wamezungumzia  zaidi  kuhusu  kupitishwa  kwa bajeti  ya  serikali  na  bunge  la  shirikisho kwa mwaka  2009, pamoja  na  mpango  wa  mafao  ya jamii  wa  umoja  wa  Ulaya.

Aliyewakusanyia  maoni  hayo  ya  wahariri  leo  hii  ni Sekione  Kitojo.


Kuhusu  kupitishwa  kwa  bajeti  ya  serikali  ya mwaka  2009  gazeti  la Westdeutsche Allgemeine Zeitung  kutoka  Essen  linathibitisha  kazi  nzuri aliyoifanyika  waziri  wa  fedha  na  kufanikisha kupitishwa  kwa  bajeti  hiyo  huku  likisema  kuwa pamoja  na  hayo  amevuka  vikwazo  vingi. Gazeti linaandika.



Iwapo Steinbrück  anajisikia  sasa  kuwa  ni   shujaa wa  sera  za   masuala  ya  fedha , itakuwa  ni  kwa muda  huu  tu , kwa  kuwa  ameweza  kufanikiwa kuzuwia   matumizi  mengine  makubwa  zaidi. Kwa hiyo  anastahili  kusifiwa. Kabla  ya  hapo  ilikuwa kuna  matumizi  makubwa. Ubanaji  wa   matumizi hata  hivyo gazeti  linasema   haukuhitaji  kuchukua hatua  nusu  nusu. Hata  hivyo  gazeti  hilo  linasema kuwa  waziri  Steinbrück  amepata  bahati  kubwa.




Katika  njia  sahihi   na   kuelekea  katika   lengo sahihi, linaeleza  gazeti  la  Nordkurier  kutoka Neubrandenburg.


Ukipima  matarajio  na  mahitaji  ambayo  wajumbe wa  baraza  la  mawaziri   walikuwa  nayo  Steinbrück amepata  matokeo  mazuri. Waziri  huyo  linasema gazeti  kuwa  amefanikiwa  kulielekeza  jahazi  katika njia  nzuri, lakini   amepoteza  muda  mrefu  kuweza kuweka    kasi  zaidi.



Gazeti  la  Der Tagesspiegel  kutoka  Berlin  linatoa sifa  kwa   serikali  ya  mseto. Linaandika.



Ni  muhimu  kwamba  Angela  Merkel  na  Peer Steinbrück   waendelee  kuzungumza   kuhusiana na  masuala  ya   upunguzaji  wa  kodi,  mafao wanayopata  wafanyakazi  wanaofanyakazi  mbali  na makaazi  yao , pamoja  na  ushuru. Tunaweza   tu kutumai  kuwa  hali   hii  haitaweza  kuingia  katika mivutano  ya  uchaguzi    ya  shirikisho  ama  ya majimbo.  Kwa  sababu  kile  ambacho  Merkel  na Steinbrück  wamekifanya  katika  kubana  matumizi na  kutokubabaika   kisiasa , kwa  kweli  ni   dhana , kwamba   sera  za   kifedha  za   Ujerumani  zitabaki kuwa  imara.





Lakini  gazeti  la  Lausitzer Rundschau  la  mjini Cottbus  linapingana  na  kila  anayefurahia muswada  wa   bajeti  uliotolewa  na  Steinbrück.


Gazeti  linasema   kuwa   katika  muda  wake madarakani  kumekuwa  na  upungufu    kuazia mwaka  2005  wa  jumla  ya  Euro  bilioni  159. Fedha hizi  zilikuwa   wapi  linauliza  gazeti  hilo.  Muungano mkuu  wa  serikali  kama  unavyoitwa  haukuweza kutumia   pato  la   ziada   na  wameendelea  tu kubana  matumizi  zaidi. Mpango  wa  Steinbrück  wa kujiondoa  kutoka  katika  madeni  hauna   umakini wowote  kama  ilivyokuwa  kwa  waziri  wa  fedha Eichel  mwaka  2002. Bado  bajeti  ina   upungufu wa  muundo  linatahadharisha  gazeti  hilo  na kusema  kuwa  bado  hakuna  kitu  cha  kujikinga  na mzozo  huu.



Suala   jingine  lililochambuliwa  na  wahariri  wa magazeti  ya  Ujerumani  ni  kuhusu   mpango  wa mafao  ya  jamii   uliotolewa  na  umoja  wa  Ulaya. Gazeti  la  Frankfurter Rundschau  limejishughulisha zaidi  na  suala  hilo.


Gazeti  linasema   kuwa  kwa  mtazamo  wake kutokana  na  lawama  kali  inabidi   mtu   kujaribu kuitetea Ujerumani. Hii  haina  maana , kwamba mipango  wa   umoja  wa   Ulaya   mjini   Brussels isitumike.  Kwa  mfano  sheria  kuhusiana  na mabaraza  ya  wafanyakazi  kwamba  inaweza kungojea  zaidi,  mpaka  pale  tume  hiyo  itakapotoa taarifa,  kuhusiana  na  kusikilizwa  kwa  maombi  ya uimarishaji  wa  wawakilishi  wa  wafanyakazi. Hata katika  suala  la  kupambana  na ubaguzi  kuna maswali  mengi  hayajajibiwa.




Gazeti  la  Leipziger Volkszeitung, linadokeza  kuwa katika  siku  za  usoni    wagonjwa  wataweza kupatiwa  matibabu   katika  mataifa , nje  ya  umoja wa  Ulaya. Gazeti  linaandika.


Lakini  gazeti  hilo  linatanabahisha   kuwa   yule ambaye  anataka   nafasi  kubwa  zaidi  ya  uchaguzi wa   kupatiwa  matibabu  hayo  nje  ya  umoja  wa Ulaya , ni  lazima  aweze  kufahamu  ni  aina  gani ya  matibabu  anaweza  kuyapata huko  na  ubora wa utendaji. Katika  baadhi  ya  nchi  kuna  upungufu mkubwa  wa  hilo. Uwanja  mpana  wa  uchaguzi kwa  wagonjwa , ambao  hadi  sasa  umetumiwa  na watu  wachache  tu , unaweza  kuanzisha mashindano  makubwa  katika  nchi  mbali  mbali , na pia utaalamu   wa  hali  ya  juu  pamoja  na  ubora zaidi.