1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri

Abdu Said Mtullya8 Aprili 2014

Wahariri wanatoa maoni juu ya maombolezo ya mauaji yaliyotokea nchini Rwanda miaka 20 iliyopita na pia juu ya mgogoro wa nchini Ukraine

https://p.dw.com/p/1Bdhz
Kikosi malumu cha kuzuia fujo nchin iUkraine
Kikosi maalumu cha kuzuia fujo nchini UkrainePicha: Reuters

Mhariri wa gazeti gazeti la "Bild" anasema matukio ya nchini Ukraine ni ya kutia wasi wasi mkubwa Watu wanaogemea upande wa Urusi, mashariki mwa Ukraine nao pia wanataka kuitisha kura ya maoni iwapo nao pia wajiunge na Urusi kama ilivyotokea kwa jimbo la Krimea. Lakini mhariri wa gazeti la Bild anauliza jee ,Rais wa Urusi, Vladimir Putin atakubali wanachokitaka watu hao? Jibu ni hapana.

Mhariri huyo anasema hiyo ndiyo sababu kwamba nchi za magharibi nazo zinapaswa kuubadilisha mtazamo wao juu ya Ukraine. Siyo jambo la busara, kuanzia usiku wa manane kuzungumzia juu ya NATO kuiunga mkono Ukraine kijeshi.

Wengine wanatengwa

Mhariri wa gazeti la "Die Rheinpfalz" anawashauri viongozi wa Ukraine wayatatue matatizo ya kisiasa ndani ya Ukraine kwenyewe. Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kwamba wafuasi wa Rais alietimuliwa, Viktor Janukovich kutoka chama kinachoegemea Urusi wanatengwa. Serikali ya Ukraine inajaribu kuwakabili wafuasi hao bila ya kutumia mabavu.Lakini hata vyama vidogo vya kisisia vina haki ya kusikilizwa.

Kiongozi wa chama kinachoegemea Urusi Dobkin amewekwa kwenye kuzuizi cha nyumbani wakati viongozi wa chama cha mrengo mkali wa kulia wanapewa uhuru wote kuendesha kampeni za kisiasa. Hata ikiwa Urusi inapiga chuku juu ya madai ya kuwapo mafashisti,karibu na serikali ya Ukraine, haifai kuyapuuza kabisa madai hayo. Gazeti la "Nürnberger Nachrichten" linasema litakuwa jambo la busara ikiwa Nato itaepuka kuziingiza katika mfungamano huo nchi zenye migogoro ya kimajimbo kama vile Ukraine.

Muhimu kukumbuka yaliyotokea Rwanda

Mhariri wa gazeti la "Süddeutsche" anazungumzia juu ya mauaji ya kimbari yalitokea Rwanda miaka 20 iliyopita.Mhariri huo anasema katika kuwakumbuka maalfu kwa maalfu waliouawa haistoshi kusikitika tu kwamba, wakati huo dunia ingeliweza kuchukua hatua za kuyapeusha mauji.

Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kwamba mafunzo yanayotokana na mauaji yaliyotokea nchini Rwanda yanasikika kutoka kila upande kwa sasa.Hata hivyo pamoja na kukumbusha kwamba jumuiya ya kimataifa ilishindwa kuyazuia mauaji miaka 20 iliyopita,inabidi sasa kuangalia mbele.

Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuzishughulikia hali zinazowakibili watu, katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini na nchini Syria. Lakini wakati huo huo ni vizuri kwamba jumuiya ya kimataifa haijayasahau yaliyotokea Rwanda.

Mwandishi:Mtullya Abdu./Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Josephat Charo