1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini.

Mtullya, Abdu Said17 Septemba 2008

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wazungumzia juu ya mswada wa bajeti.

https://p.dw.com/p/FJmZ
Waziri wa fedha P. Steinbrück na mwenzake wa uchumi Michael Glos wakisikiliza mjadala wa bajeti bungeni.Picha: AP

Katika maoni yao,  wahariri  wa magazeti leo wanazungumzia  juu ya bajeti ya Ujerumani kwa kipindi  kijacho cha fedha.

Waziri wa  fedha wa Ujerumani  bwana Peer Steinbrück  amewasilisha  mswada wa bajeti ya Euro Bilioni 288.4  kwa ajili ya mwaka ujao wa  fedha. Maoni yanatofautiana juu ya  bajeti hiyo.

Mhariri  wa  gazeti  la Reutlinger General  Anzeiger  anatilia maanani kwamba bajeti  hiyo imevunja  rekodi. Kwani waziri  wa fedha bwana Steinbrück ameongeza   bajeti hiyo kwa Euro 5.2

Lakini mhariri anasema pia inapasa kutilia  maanani  vilevile kwamba  ,katika mwaka  ujao serikali kuu ya Ujerumani itapaswa kutenga kiasi cha Euro bilioni 42.5  kwa ajili ya kulipia riba.

Serikali ya Ujerumani inadaiwa  jumla ya Euro bilioni 920.


Mhariri wa gazeti  la Neue Osnabrücker haoni afueni yoyote  katika mswada wa bajeti uliowasilishwa na waziri Steinbrück japo lengo la waziri huyo wa fedha ni kupunguza deni la serikali.

Gazeti hilo linatilia  maanani  kwamba wakati waziri  huyo  anataka kupunguza deni, matumizi  yataongezeka kwa Euro bilioni 5.2 Mhariri wa  gazeti anasema mambo hayo  mawili  hayawezi kuenda sambamba  hasa wakati huu ambapo pana  wasiwasi  juu ya ustawi  wa uchumi  kutokana na mgogoro  wa fedha  nchini Marekani.

Gazeti la Schwäbische linasema  lengo la kuwa na bajeti yenye  urari lazima lifikiwe na wabunge wa vyama vyote vilivyomo katika serikali ya mseto, la sivyo hapatakuwa na sababu  kwao , kuendelea kuwapo.

Mhariri  wa gazeti hilo  anawazungumzia wabunge wanaotaka kupunguza  kodi badala  ya kupunguza deni la serikali, bila ya kuzingtia ukweli  kwamba  deni  la leo ndiyo kodi ya kesho.

Lakini mhariri wa gazeti la Mitteldeutsche anampongeza waziri wa  fedha kwa kusema ukweli juu ya  bajeti.

Gazeti linatilia maanani kuwa waziri huyo hakutoa  ahadi  zozote kwa wananchi alipowasilisha  mswada wa bajeti. Mhariri anaeleza kuwa kuongezeka bei za nishati  na  chakula siyo  mambo ya kupita,bali ni matokeo ya sera  za dunia utandawazi. Bei ya nishati inapanda kutokana  na ongezeko la mahitaji katika nchi  kama  China na  Brazil- katika  hali hiyo ruzuku  za serikali hazitasaidia. Gazeti linasema hiyo ndiyo sababu kwamba waziri wa fedha  bwana Steinbrück amepinga vikali wazo juu ya serikali  kutoa ruzuku