1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni:Eti Francis ni Papa wa muda tu?

15 Machi 2013

Papa Francis wa kwanza,kutokana na umri wake mkubwa na mwelekeo wake wa kihafidhina,haonyeshi kama atafanikiwa kulifanyia mageuzi kanisa katoliki,yanayoambatana na wakati tulio nao.

https://p.dw.com/p/17xWt
Klaus KrämerPicha: DW

Wahenga wanasema mkamia maji hayanywi" hapa ikimaanisha anaeingia katika mkutano wa siri akipewa  nafasi nzuri ya kuchaguliwa kuwa Papa,anatoka mkutanoni kama kadinali tu.Kwasababu hakuna yeyote kati ya waliopigiwa upatu wangechaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni,aliyechaguliwa-badala yake makadinali wamemchagua mchamungu ambae amejipatia umashuhuri kutokana na kutopenda makubwa pamoja na juhudi zake za kuwapigania wasiojiweza .Kardinali wa ki-Argentina Jorge Mario Bergoglio,aliyechagua jina la Francis wa kwanza,ni Papa wa kwanza ambae hatokei Ulaya.Nchini mwake,amedhihirisha anapenda sana kuwa karibu na watu na anazijua kikamilifu dhiki na shida za watu maskini.Hilo pekee linawapa matumaini mema wakatoliki wanaoishi katika maene ya mabanda,madongo poromoka na kambi za wakimbizi katika kila pembe ya dunia.Katika eneo la Latin Amerika matumaini yalikuwa makubwa ya kumpata Papa anaetambua hali zao za maisha.

Hata mrithi huyu wa sasa wa mjumbe wa Mungu Petrus ni mhafidhina- jambo ambalo si la kustaajabisha - watangulizi wake wote wawili na kwa kipindi cha miaka 35 iliyopita walikuwa wakiwachagua maaskofu wakuu wa kihafidhina  kuwa makadinali na kwa namna hivyo kuwapatia fursa ya kumchagua Papa.Francis wa kwanza kwa hivyo hawezi kuwa mwanamageuzi ambae wakosoaji wa kanisa wangependelea achaguliwe.Muumini huyo wa madhehebu ya Jesuit anaitumia kila fursa inayojitokeza kukosoa kwa maneno makali ukosefu wa usawa katika jamii-hata hivyo yeye mwenyewe anatajikana kuwa karibu zaidi na jumuia ya wahafidhina sugu wa kikatoliki:"Comunione e Liberazione".Theolojia ya ukombozi" haikuwa shetani wake.Sasa jee Papa kama huyu anaweza kuyawekea suala la kuuliza mafunzo ya dini ya kikatliki?

Na jee watu wanaweza kumpongeza Papa huyu?

Majukumu na matatizo yanayomsubiri mchamungu huyo mwenye umri wa miaka 76 ni makubwa kupita kiasi.Kwanza kabisa Papa Francis wa kwanza anabidi arejeshe imani ya waumini.Kashfa ya kuingiliwa kimwili watoto na vijana na wachamungu wa kikatoliki kimechafua sana hadhi ya kanisa na hasa katika nchi za magharibi ambako umati wa waumini wanalipa kisogo kanisa.

Francis wa kwanza analazimika kuanzisha mageuzi yanayohitajika ya kanisa na ambayo yalikuwa yaanze tangu zamani.Kuna suala la kuwepo  tabaka mbili za jamii kati ya maaskofu na watu wanaojitolea kulitumikia kanisa,sura hiyo inabidi ibadilishwe na kuimarisha nafasi ya waumini wanaolitumikia kanisa kwa kujitolea.Wakinamama, ambao ndio wanaotekeleza sehemu kubwa ya shughuli za kanisa wanastahiki kuzingatiwa.Mjadala wa uwazi kwa wale wanaounga mkono na wengine wanaopnga utawa unabidi uendelezwe.Kitheolojia watu wanasubiri pia kuona vipi litashughulikiwa suala la watu walioachana na kuowa au kuolewa na mtu mwengine.Uhusiano pamja na makanisa ambayo si ya kikatoliki na hasa yale ya wapenda mageuzi nao ia unahitaji kuchunguzwa.Mdahalo kati ya waumini wa dini tofauti unabidi uendelezwe na mengi menginyo.

Si wa kumezewa mate

Lakini hata Vatikan kwenyewe kuna yanayobidi kushughulikiwa.Kashfa ya kuibiwa hati za siri za Papa,visa vya kichini chini vya hadaa na kutiliana fitna yote hayo yamezidisha dhana kwamba Papa Benedkt wa 16 alishindwa kuidhibiti hali ya mambo.

Hasha,hakuna anaeumezea mate wadhifa wa kiongozi wa wakatoliki bilioni moja nukta mbili.Pekee umri wake mkubwa unamfanya mtu ashuku kama kweli yeye ndie anaefaa.Yadhihirika zaidi kana kwamba makadinali wamemchagua Papa wa kipindi cha mpito na wala hawajachagua mkonndo mpya.Pengine mkutano wa siri,kutokana na hali inayolikabili kanisa katoliki imeipoteza fursa iliyojitokeza.Lakini si kuna usemi usemao imani huzusha miujiza.

Mwandishi:Krämer,Klaus/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman