1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapambano bado yanaendelea Basra na Baghdad.

27 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DVpS

Baghdad.

Wanamgambo wa Kishia wameendelea kurusha makombora na mizinga katika eneo linalolindwa sana la ukanda wa kijani mjini Baghdad leo.

Katika siku ya nne ya mashambulio, moshi uliweza kuonekana ukitoka katika majengo ya ofisi za serikali ya Iraq na ubalozi wa Marekani.

Hakuna watu walioripitiwa kujeruhiwa.

Msemaji wa jeshi la Marekani meja jenerali Kevin Bergener amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Baghdad kuwa mapambano ya majeshi ya serikali mjini Basra ni njia ya kutaka kurejesha hali ya udhibiti kwa serikali.

Jeshi la Marekani linalaumu kikundi cha watu wenye imani kali wanaomuunga mkono kiongozi wa kidini Muqtada al-Sadr.

Maafisa mjini Baghdad wanafanya mazungumzo na wasaidizi wa karibu wa al-Sadr katika mji wa Najaf katika juhudi za kumaliza mzozo wa hivi sasa katika mji wa kusini wa bandari wa Basra ambako majeshi ya Iraq yanapambana na wanamgambo wa Kishia.