1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yazuka Port Harcourt.

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CizV

Abuja. Kiasi watu 13 wameuwawa katika mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji katika eneo linalotoa mafuta nchini Nigeria la Port Harcourt. Msemaji wa jeshi la nchi hiyo amesema kuwa kundi la watu wenye silaha lilishambulia vituo viwili vya polisi na kuvamia hoteli moja. Shambulio hilo limekuja siku chache baada ya majeshi ya serikali kushambulia kwa mabomu maeneo ya maficho ya waasi karibu na mji huo.

Pia yanafuatia kuvunjika kwa mazungumzo ya amani baina ya wapiganaji hao na serikali.