1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPUTO:Dawa zauzwa kimagendo

24 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWO

Idadi kubwa ya dawa zilizoagizwa nchini Msumbiji na jamii ya kimataifa zinaripotiwa kuuzwa katika masoko yasiyo rasmi nchini humo na mataifa mengine ya kigeni.Hayo ni kwa mujibu wa waziri wa Afya wa Msumbiji Ivo Garrido.

Waziri huyo anaongeza kuwa baadhi ya dawa hizo zinauzwa kinyume na sheria katika sekta isiyo rasmi nchini Msumbiji.Kiongozi huyo anatoa wito kwa wafanyikazi wa serikali aidha wakazi wa nchi kuarifu polisi wakati wowote wanaposhuhudia kisa cha wizi wa dawa hizo.