1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani, Canada, Kenya zaunga mkono kupunguza hewa chafu

Bruce Amani
6 Desemba 2023

Marekani, Canada na Kenya ni miongoni mwa nchi 63 zilizounga mkono ahadi ya kupunguza kwa kiwango kikubwa gesi zinazochafua mazingira, katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu tabia nchi unaoendelea Dubai.

https://p.dw.com/p/4Zpew
Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Mabadiliko ya Tabianchi, John Kerry.
Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Mabadiliko ya Tabianchi, John Kerry.Picha: Amr Alfiky/REUTERS

 Ahadi ya kupunguza viwango vya joto duniani, inaashiria lengo la kwanza la pamoja la kimataifa kuhusu uchafuzi unaosababisha ongezeko la joto duniani kupitia gesi chafu zinazotoka kwenye vifaa vya upozaji  ambavyo ni pamoja na majokofu ya vyakula na dawa na viyoyozi.

Soma zaidi: UN: Kuelekea COP28 ulimwengu wapambana na mafuta ya visukuku

"Kuna takriban nchi 195 hapa na kuna watu ulimwenguni kote, ambao wanategemea sisi sote kufanya maamuzi haya. Kwa hivyo wacha tuungane pamoja kuwa waeneza kampeni, watu ambao wako tayari kupigania mabadiliko haya kwa kasi zaidi. Tuna uwezo wa kuokoa maisha." Alisema John Kerry, mjumbe maalum wa Marekani kuhusu tabianchi.

Soma zaidi: Ruto asema mabadiliko ya tabianchi yanatafuna maendeleo ya Afrika

Ahadi hiyo inazitaka nchi kupunguza ifikapo mwaka wa 2050 uchafuzi wao unaotokana na teknolojia ya upozaji kwa karibu asilimia 68 ikilinganishwa na viwango vya mwaka wa 2022.