1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Marekani na Kenya wasaini makubaliano ya ulinzi

Lilian Mtono
26 Septemba 2023

Marekani na Kenya wamesaini makubaliano ya ulinzi yatakalisaidia taifa hilo la Afrika Mashariki kupata vifaa na msaada kwa wanajeshi wakati taifa hilo likijiandaa kuongoza ujumbe wa kimataifa wa amani nchini Haiti.

https://p.dw.com/p/4WnmQ
Moja ya makundi ya uhalifu katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince linaloongozwa na aliyewahi kuwa afisa wa polisi Jimmy "Barbecue" Charizier(katikati). Mji huo unakabiliwa na machafuko ya makundi hayo yanayotaka serikali ijiuzulu.
Moja ya makundi ya uhalifu katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince linaloongozwa na aliyewahi kuwa afisa wa polisi Jimmy "Barbecue" Charizier(katikati). Mji huo unakabiliwa na machafuko ya makundi hayo yanayotaka serikali ijiuzulu.Picha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Haiti inapambana na machafuko yanaoyasababishwa na makundi ya uhalifu na hasa katika mji mkuu Port-au-Prince.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesaini makubaliano hayo na mwenzake wa Kenya Aden Duale katika mkutano uliofanyika Nairobi.

Makubaliano hayo ni yanaongoza uhusiano wa kiulinzi kwa miaka mitano ijayo wakati taifa hilo likiongeza harakati zake dhidi ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab zikiongezeka.

Austin ameishukuru Kenya kwa kujitolea kuongoza ujumbe wa amani nchini Haiti na kusema kwa mara nyingine kwamba serikali ya Marekani itashirikiana na Bunge ili kupata dola milioni 100 za ufadhili ilizoahidi pembezoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.