1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yavishambulia vituo vya silaha Syria

Bruce Amani
27 Oktoba 2023

Marekani imevishambulia vituo vya silaha nchini Syria kama hatua ya kulipiza mashambulizi dhidi ya askari wa Marekani yaliyofanywa na wanamgambo wanaooungwa mkono na Iran.

https://p.dw.com/p/4Y6HG
Rais wa Marekani Rais Joe Biden
Rais wa Marekani Rais Joe BidenPicha: Jonathan Ernst/AFP

Hayo yanajiri wakati wasiwasi ukiongezeka kuwa mzozo kati ya Israel na Hamas huenda ukasambaa katika kanda wa Mashariki ya Kati.

Rais Joe Biden wa Marekanialiamuru mashambulizi hayo yaliyofanywa na ndege mbili za kivita kwenye vituo viwili vinavyotumiwa na jeshi la walinzi wa mapinduzi la Iran na makundi ya wapiganaji linaloyaunga mkono.

Soma pia:Biden: Kufanikiwa kwa Ukraine na Israel katika vita vyao ni muhimu kwa usalama wa Marekani

Askari wa Marekani na jeshi la muungano wameshambuliwa karibu mara 19 nchini Iraq na Syria na vikosi vinavyoungwa mkono na Iran katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Makundi ya Hamas, Islamic Jihad na Hizbullah la Lebanon yote yanaoungwa mkono na Tehran.