1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kupunguza ruzuku ya kilimo kwa dolla billioni 2.0

22 Julai 2008

Brazil yasema hatua hiyo ya Marekani ni dhaifu

https://p.dw.com/p/EhuK
Vikao vya mazungumzo ya WTO vyaendeleaPicha: AP

Marekani imejitolea kupunguza ruzuku ya mwaka ya wakulima wake kutoka dolla bilioni 2.0 hadi dolla billioni 15 katika juhudi zakuyasukuma mbele mazungumzo yanayoendelea ya shirika la bishara duniani WTO.Hata hivyo Brazil inasema hatua hiyo ya Marekani haitoshi.

Kwa Upande mwingine kamishna mkuu wa Umoja wa Ulaya anasehusika na masuala ya biashara Peter Mandelson amesema tangu mwanzo kwenye mkutano huo kwamba Umoja huo utabidi kupunguza kwa asilimia 60 ruzuku ya kilimo ikiwa washiriki wengine kwenye mazungumzo hayo watafanya juhudi kubwa.

Kupunguzwa ruzuku ndio suala kubwa ambalo nchi za Afrika zinataka lipatiwe ufumbuzi.

Kwa muda wa miaka sabaa sasa shirika hilo la biashara duniani WTO limekuwa likitafuta ufumbuzi wa kuweka kanuni za kibiashara duniani.

Na masuala muhimu miongoni mwao ambayo yanazusha utata kati ya wanachama wa shirika hilo la WTO ni kupunguzwa kwa kiwango cha ushuru wa bidhaa za viwandani na ruzuku ya kilimo.

Wakulima wa nchi 30 zilizoendelea kiuchumi mwaka jana walipokea msaada wa ruzuku ya kiasi cha dolla billioni 258 kiwango ambacho kwa hakika ni robo ya mapato ya wakulima hao.

Kwa hivyo kutokana na hali hiyo afisa wa Umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya kilimo Martin Gore anasema kilimo katika nchi za Afrika ni duni na anaendelea kusema.

''Kizingiti kikubwa na muhimu kwa nchi nyingi za kiafrika ni hasa suala la nchi tajiri kupunguza ruzuku ya bidhaa za kilimo katika nchi hizo.''

Aidha afisa huyo wa Umoja wa Mataifa Martin Gore anasema nchi za Kiafrika zimekuwa zikijikuta mara nyingi kwenye ushindani mkubwa wa kibiashara kutoka mataifa tajiri.Anasema

''Nchi nyingi za kiafrika zimejiingiza katika biashara huru halafu zinakumbana na ushindani usiokuwa wa haki.

Kwa mfano nilikuwa nchini Sierreleone miaka ya hivi karibuni na ungeweza kununua mchele mjini Freetown ambao umetoka Thailand kwa bei nafuu kabisa kuliko mchele uliolimwa Sierreleon.''

Katika mazungumzo yanayoendelea mjini Geneva Uswisi mjumbe wa Marekani Susan Schwab amesema nchi yake iko tayari kupunguza kiwango cha ruzuku ya wakulima wake ya kila mwaka kutoka dola billioni 2.0 hadi dolla billioni 15.

Brazil inasema hatua hiyo haitoshi Marekani inabidi kuchukua hatua zaidi.Marekani imetoa pendekezo hilo ili nayo kwa upande mwingine ifunguliwe milango ya masoko kwa bidhaa zake za viwandani katika nchi zinazoinukia kiuchumi.

Kwa upande mwingine shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake mjini Geneva Usiwsi ambalo ni taasisi ya sera za kilimo na biashara IATP pia linasema pendekezo hilo la Marekani ni dhaifu mno.

Taasisi hiyo inasema Marekani inaomba kinga ya kuepuka kukabiliwa na changamoto za kisheria katika shirika la WTO na pia inataka kupata nafasi ya kuingiza kwenye masoko ya nchi zingine bidhaa zake za kilimo na viwandani kwa njia rahisi.