1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroNiger

Niger yajadiliana na Marekani juu ya kuondoa wanajeshi wake

Lilian Mtono
25 Aprili 2024

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema maafisa wake watakutana hii leo na wajumbe wa serikali ya Niger mjini Niamey kujadili juu ya kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger.

https://p.dw.com/p/4f9mt
Niger | Wanajeshi wa Marekani wakiwa mafunzoni
Wanajeshi wa Marekani katika picha iliyopigwa Februari 2, 2020 huko agadez, Niger. Taifa hilo sasa linataka wanajeshi hawa waondoke nchini humoPicha: Alex Fox Echols Iii/Planet Pix/ZUMA Wire/picture alliance

Utawala wa kijeshi wa Niger umeiomba Marekani kuwaondoa wanajeshi wake waliomo nchini humo kutokana na kutoelewana kuhusu masuala kadhaa ambayo ni pamoja na kushindwa kutambua hatua zilizopigwa na taifa hilo kuelekea utawala wa kidemokrasia. 

Hadi mapinduzi ya mwaka jana Niger ilikuwa mshirika mkubwa wa Marekani katika vita dhidi ya ugaidi na wanajeshi hao wamekuwa wakitoa mafunzo kwa vikosi vya nchini humo kupambana na makundi ya wanamgambo.

Chanzo chenye uelewa na suala hilo wiki iliyopita kilisema Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Kurt Campbell na utawala wa Niger wamekubaliana juu ya hatua hiyo.