1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaahirisha mkutano wa VVU/UKIMWI nchini Uganda

27 Aprili 2023

Marekani imeahirisha mkutano kuhusu mpango wa VVU/UKIMWI uliotarajiwa kufanyika nchini Uganda, ikisema wanahitaji muda wa kutathmini athari za muswada wa kupinga watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

https://p.dw.com/p/4QdO9
Uganda | LGBTQ Gesetz
Picha: Abubaker Lubowa/REUTERS

Mpango huo wa PEPFAR unaotumia dola milioni 400 kwa mwaka nchini Uganda, mapema wiki hii uliwaarifu washirika wake kwamba mkutano huo uliahirishwa kutokana na uwezekano wa kusainiwa kwa sheria hiyo. 

Soma pia: Uganda yapata shinikizo kimataifa kuhusu muswada dhidi ya LGBTQ

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema mapema leo kwamba uamuzi huo haulengi kusimamisha ufadhili ama kupunguza huduma, na badala yake utatoa nafasi kwa maafisa kutathmini athari za sheria hiyo dhidi ya mpango huo wa PEPFAR.

Muswada huo unaotajwa kuwa na adhabu kali zaidi, dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda ulipitishwa na bunge Machi 21, lakini ulirejeshwa bungeni na rais Yoweri Museveni akitaka urekebishwe.