1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi dhidi ya wanajeshi Jordan lilipangwa- Marekani

1 Februari 2024

Marekani imesema shambulizi la droni lililowauwa wanajeshi wake watatu huko Jordan lilifanywa na wanamgambo wa Iraq wanaoungwa mkono na Iran, wakati ambapo Rais Joe Biden anatafakari kuhusu kujibu shambulizi hilo.

https://p.dw.com/p/4buTB
Washington, Marekani | Msemaji wa Baraza la Kitaifa la Usalama John Kirby
Msemaji wa Baraza la Kitaifa la Usalama Marekani John KirbyPicha: Chris Kleponis/UPI Photo/IMAGO

Msemaji wa Baraza la Kitaifa la Usalama John Kirby amesema Marekani inaamini shambulizi lilipangwa na kufadhiliwa na kundi la Islamic Resistance huko Iraq ambalo linajumuisha kundi la Kataib Hezbollah.

Kufikia jana, Kataib Hezbollah na makundi mengine ya wanamgambo yanayoungwa mkono na Iran yalikuwa yamefanya mashambulizi 166 dhidi ya majeshi ya Marekani.

Soma pia:Rais wa Marekani Joe Biden azidi kushinikizwa kisiasa kuchukua hatua dhidi ya moja kwa moja dhidi ya Iran

Marekani imejibu mara kadhaa mashambulizi ya wanamgambo hao katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.