1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaidhinisha msaada kwa Ukraine, Taiwan na Israel

24 Aprili 2024

Baraza la Seneti la Marekani limeidhinisha kitita cha msaada wa dola bilioni 61 kwa ajili ya Ukraine, huku rais Joe Biden akiahidi kuutia saini haraka muswada huo uliocheleweshwa kwa muda mrefu.

https://p.dw.com/p/4f7ps
Marekani/ Ukraine
Kifurushi cha msada huo kilipitishwa kwa kura nyingi katika Baraza la SenetiPicha: Nathan Howard/Getty Images

Sehemu ya msaada huo ambao kwa jumla ni dola bilioni 95, unatarajiwa kuelekezwa Taiwan na Israel, huku kifurushi hicho pia kikitenga fedha za msaada wa kibinaadamu unaohitajika kwa Gaza, Sudan na Haiti.

"Tunawaambia washirika wetu tunasimama nanyi. Tunawaambia wapinzani wetu, msitujaribu. Tunauambia ulimwengu, Marekani itafanya kila kitu kulinda demokrasia na mtindo wetu wa maisha. Muswada huu ni mojawapo ya hatua kubwa kabisa kuwahi kuidhinishwa na bunge kwa miaka mingi kwa dhamira ya kulinda usalama wa Marekani na hatma (yetu) ya siku zijazo."

Baraza la Seneti la Marekani laidhinisha msaada kwa Ukraine

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameipongeza hatua hiyo ambayo inalenga kulisaidia taifa lake kukabiliana na uvamizi wa Urusi. 

Kupitia mtandao wa kijamii wa X, Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Israel Katz ameshukuru hatua hiyo akisema ni ushuhuda wa wazi wa ushirika wake na Marekani na unatuma ujumbe mzito kwa "maadui wake."