1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yamuuwa kiongozi wa IS Somalia

Mohammed Khelef
16 Aprili 2019

Jeshi la Marekani lilithibitisha kumuua kiongozi wa pili katika uongozi wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) nchini Somalia katika shambulizi lake la anga.

https://p.dw.com/p/3GtiU
Afrika Senegal US Soldaten
Picha: Getty Images/AFP/Seyllou

Jeshi hilo la Marekani barani Afrika (AFRICOM) lilisema Abdulhakim Dhuqub aliuawa siku ya Jumapili katika mkoa wa Bari. 

Katika tathmini ya sasa, jeshi hilo lilisema shambulizi hilo lilimuua kiongozi huyo pekee sambamba na kuharibu gari moja.

Dhuqub alikuwa akihusika na operesheni za kila siku za kundi hilo la wanamgambo, ikiwemo kupanga mashambulizi na kufanya manunuzi. 

Kundi la IS lina operesheni chache  nchini Somalia, ambako wapiganaji wa al-Shabab wana nguvu na wana mafungamano na mtandao wa al-Qaida.