1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasema haitokuwa kikwazo katika makubaliano ya Bali

4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWTv

BALI.Wajumbe wa Marekani katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali hewa uliyoanza jana huko Bali Indonesia wamesema kuwa nchi hiyo haitakuwa kikwazo katika kufikia makubaliano mapya juu ya upunguzaji wa gesi ya cabon.

Zaidi ya wajumbe elfu 10 kutoka nchi 190 duniani wanajadili njia ya kuelekea katika mazungumzo ya kuundwa kwa mkataba mpya wa hali ya hewa kuchukua nafasi ya ule wa Kyoto unaomalizika mwaka 2012.

Marekani ni nchi pekee tajiri kiviwanda ambayo haijaridhia mkataba huo wa Kyoto unaotaka kupunguzwa kwa matumizi ya gesi inayoongeza joto duniani..