1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatafuta kuwanusuru maelfu Iraq

Admin.WagnerD13 Agosti 2014

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Jonh Kerry amesema kwa hivi sasa wanaangalia uwezekano wa haraka wa kuwanusuru raia waliokwama katika maeneo ya milima huko kaskazini mwa Iraq.

https://p.dw.com/p/1CtNP
Irak Flüchtlinge 10.08.2014 Sindschar Gebirge
Wairaq katika maeneo ya milima SanjirPicha: Reuters

Maelfu ya watu wa jamii ya wacahche iitwayo Yazidi na Wakristo, wanaendelea kukabiliwa na kitisho cha kundi la wapiganaji wa jihadi IS na kuashiria kitisho kibaya zaidi ja janga la kibinaadamu. Awali Umoja wa Mataifa ulisema kati ya jamii hiyo ya watu 20,000 mpaka 30,000 wamekwama katika mlima Sinjar, na mtaalamu wa haki za binadamu kwa kundi hilo la wahache wa Umoja wa Mataifa, Rita Izsak alionya uwezekano wa kukabiliwa ukatili wa jumla au mauwaji ya halaiki katika kipindi cha siku chache au masaa.

Kundi hilo kubwa la watu katika lililojificha katika mlima Sinjar, wamekwama katika eneo hilo lililokuwa na joto kali la msimu wa kiangazi pasipo vyakula vya kutosha wala maji ya kunywa.

Jitihada za kutoa misaada zaendelea

Marekani imekuwa ikiongoza jumuiya ya kimataifa katika kuongeza kufanikisha misaada ya kiutu kwa watu wote waliokwamishwa katika ukanda wa Kikurd, na kwamba waziri Kerry amesema namna ya kuwaokoa watu hao katika eneo hilo bado ipo katika meza ya majadiliano.

Irak Flüchtlinge Jesiden Sindschar Gebirge 11. August
Wakimbizi wa Iraq kutoka milima ya SanjirPicha: Reuters

Akiwa katika mji mkuu wa Visiwa vya Solomon, Honiara aliwaambia waandishi habari kwamba wanafanya haraka sana na kutoa uwamuzi mgumu kwa kuwa ni jambo la dharura sana kujaribu kuwanusuru watuo hao katika maeneo ya milima.

Marekani yaongeza wanajeshi nchini Iraq

Chack Hagel ni waziri wa ulinzi wa Marekani. "Nimependezea kwa rais na rais amenipa ridhaa ya kuendelea kupeleka tumu mpya wanajeshi 130 ili kwenda kutathimi wapi tunaweza kuwasaidia Wairaq katika kile walichokua wanakifanya na hasaka katika kitisho hicho wanachokabiliana nacho sasa".

Nchini Iraq katika jitihada za kuinusuru jamii hiyo ya watu helkopta iliyobeba misaada jana ilipata ajali wakati kianza kupaa na kusababisha kifo cha rubani na kumjeruhi mbunge wa jamii ya Yazidi Vian Dakhil. Gazeti la New York Times liliripoti kuwa mwandishi wake alikuwemo katika chombo hicho amejeruhiwa vibaya.

Jeshi la Marekani limesema limefanya awamu sita za kuangusha misaada katika eneo hilo ambapo wamefanikiwa kuangusha mafurushi 108 ya vyakula na maji katika eneo la mlima wa Sinjar.

Na katika hatua nyingine kiongozi wa juu kabisa wa kidini wa Misri, Mufti Shawki Allam amelilaani kundi la Taifa la Kiislamu kwa kuliita kundi la kigaidi ambalo linasababisha hatari kwa Uislamu na Waislamu.

Baada ya kuteka sehemu kubwa ya kaskazini mwa mji wa Mosul mapema Juni na kuyadhibiti pia maeneo ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni, wapiganaji hao wameanzisha mashambulizi mingine makali mwezi huu. Wameshambulia jamii ya wachache ya Kikristo, Yazidi, Waturuki na Shabak katika maeneo ya magharibi, kaskazini na mashariki mwa Mosul na kuzusha maafa makubwa.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP
Mhariri: Josephat Charo