1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yawapa mafunzo askari wa Ukraine nchini Ujerumani

17 Januari 2023

Jeshi la Marekani limeanza kuwapa mamia ya wanajeshi wa Ukraine mafunzo mapya ya pamoja ya matumizi ya silaha. Mwanajeshi wa cheo cha juu wa Marekani, Jenerali Mark Milley, alizuru eneo la mafunzo hayo la Grafenwöhr

https://p.dw.com/p/4MILl
Deutschland Grafenwöhr | Übung Bradley Schützenpanzer
Picha: US Army/ZUMA Wire/IMAGO

Hapo jana, mwanajeshi wa cheo cha juu wa Marekani, Jenerali Mark Milley, alizuru eneo la mafunzo hayo la Grafenwöhr nchini Ujerumani, karibu na mpaka na Jamhuri ya Czech.

Vikosi vya Ukraine vimepokea mafunzo katika eneo hilo kuhusu mifumo ya silaha mbalimbali ambazo zilitolewa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, tangu Urusi ilipoivamia Ukraine Februari mwaka uliopita.

Milley aliwaambia waandishiwa  habari walioambatana naye kwenye ziara hiyo kuwa ana matumaini silaha mpya ambazo Ukraine imeahidiwa zitakuwa tayari kutumika kabla ya kuanza kwa mvua za majira ya machipuko.