1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yawarejesha wahamiaji 50 Haiti

19 Aprili 2024

Marekani imewarudisha zaidi ya wahamiaji 50 kutoka nchini Haiti, taifa ambalo limekuwa likikabiliwa na ongezeko la ghasia za magenge ya uhalifu katika siku za hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4ex8N
Haiti
Bendera ya Haiti, taifa ambalo limelemewa na makundi ya wahalifu.Picha: H. Tschanz-Hofmann/IMAGO

Msemaji wa Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani amesema sera ya taifa lake haiwaruhusu watu ambao si raia na wasio na msingi wa kisheria kusalia nchini humo.

Afisa mmoja wa masuala ya uhamiaji nchini Haiti ameliambia shirika la habari la AFP kwamba jumla ya raia 52 wa Haiti waliwasili katika uwanja wa ndege wa mji wa Cap-Haitien siku ya Alhamisi (Aprili 18).

Soma zaidi: Marekani yawarudisha zaidi ya wahamiaji 50 kutoka Haiti

Tangu mwishoni mwa mwezi wa Februari, magenge ya uhalifu yenye nguvu yameungana kuanzisha mashambulizi kote nchini humo, ikiwemo vituo vya polisi na magereza na kusababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Ariel Henry.

Kutokana na mzozo huo unaozidi kuwa mbaya, karibu mashirika 500 ya kutetea haki za binadamu mwezi uliopita yaliandika barua iliyotumwa kwa maafisa wa Marekani, akiwemo Rais Joe Biden, wakiomba kusitishwa mpango wa kuwarudisha nyumbani wahamiaji kutoka Haiti.