1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UgaidiAfrika

Marekani yawawekea vikwazo viongozi wa makundi ya kigaidi

24 Aprili 2024

Marekani imewawekea vikwazo viongozi wa makundi ya wanamgambo katika eneo la Afrika Magharibi kutokana na vitendo vyao vya kuwachukua watu mateka ikiwa ni pamoja na Wamarekani.

https://p.dw.com/p/4f75Q
Mapambano dhidi ya Ugaidi katika kanda ya Sahel
Wanajeshi wakiwasaka wanamgambo wa makundi ya kigaidi huko Burkina FasoPicha: Philippe De Poulpiquet/MAXPPP/dpa/picture alliance

Vikwazo hivyo viliwalenga viongozi wa tawi la kundi la kigaidi la al-Qaeda huko Afrika Magharibi liitwalo Jama'at Nusrat al-Islam wal Muslimeen (JNIM), pamoja na Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Mourabitoun.

Kwa miaka kadhaa sasa, nchi za Afrika Magharibi zimekuwa zikikabiliwa na uasi wa makundi yenye itikadi kali za Kiislamu ambayo yalikita mizizi nchini Mali mnamo mwaka 2012, na kutanua udhibiti wao katika  eneo la Sahel  licha ya juhudi za kijeshi zinazoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.