1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yawawekea vikwazo maafisa wa Uganda na Zimbabwe

5 Desemba 2023

Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo vya visa maafisa kadhaa wa Uganda wakiwemo wale inaoamini wanahusika kuhujumu demokrasia na kuwakandamiza makundi ya watu wanaotengwa.

https://p.dw.com/p/4ZmZZ
Anti LGBTQ Protests I Kenya Gay Rights
Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Hatua kama hiyo imechukuliwa pia kwa maafisa wa Zimbabwe. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alipotangaza hatua hiyo, hakutaja jina la mtu yeyote lakini amesema miongoni mwa wanaotengwa au kukandamizwa ni jamii ya watu wanaodiriki mapenzi ya jinsia moja (LGBT) nchini Uganda, wanahabari, wanaharakati wa mazingira na wawakilishi wa mashirika ya kiraia nchini Zimbabwe.Sheria dhidi ya mashoga nchini Uganda inachukuliwa kuwa moja ya sheria kali zaidi duniani huku Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akikabiliwa na ukosoaji mkubwa baada ya kushinda muhula wa pili katika uchaguzi wenye utata mwezi Agosti.