1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Martine Aubry ashindwa: Francois Hollande ndiye mgombea wa urais

Thelma Mwadzaya17 Oktoba 2011

Mwanasiasa mkongwe wa chama cha Kisoshalisti cha Ufaransa, Francois Hollande, ndiye mgombea wa urais katika uchaguzi utakaofanyika mwakani.

https://p.dw.com/p/12t7W
Francois HollandePicha: AP

Bwana Francois Hollande aliibuka mshindi kwenye uchaguzi wa hapo jana Jumapili baada ya kuchuana na meya wa mji wa Lille na Waziri wa kazi wa zamani wa Ufaransa, Martine Aubry.

Frankreich Parlamentswahlen Sozialisten Francois Hollande
Francois Hollande kwenye kampeniPicha: AP

Hii ni mara ya kwanza kwa uchaguzi wa aina hiyo kufanyika nchini Ufaransa. Duru zinaeleza kuwa Francois Hollande aliye na msimamo wa wastani analiunga mkono suala la Ufaransa kuwa na ushirikiano wa karibu zaidi na mataifa mengine ya bara la Ulaya.

Pindi baada ya kuipiga kura yake, Bwana Hollande alisema kuwa chama chake cha Kisoshalisti kimeuanza mchakato wa kuhakikisha kuwa mgombea wake anaibuka mshindi katika uchaguzi wa rais ujao.

Frankreich Regionalwahlen Martine Aubry
Martine Aubry akizungumza na waandishi wa habariPicha: AP

Itakumbukwa kuwa chama hicho kilipata ushindi wa aina hiyo kwa mara ya mwisho mwaka 1988. Kulingana na kura ya maoni, Francois Hollande huenda akampiku Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy endapo uchaguzi ungefanyika wakati huu.

Mwandishi: Mwadzaya, Thelma-ZPR