1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Masaa 24 ya mwisho ya kuweka chini silaha Gaza

Admin.WagnerD7 Agosti 2014

Waziri katika serikali ya Israel ameonya kuwa taifa lake litajibu mapigo endapo kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas litaanza mapigano baada ya hatua ya usitishwaji wa muda mfupi wa mapigano katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/1Cqjg
Gaza Zerstörung Alltag 6. August
Mpanaa baskeli akipata fursa ya kuzuguka mitaaniPicha: Reuters

Kauli hiyo inakwenda sambamba na ile ya awali ya kitisho cha Hamas dhidi ya Israel, inayonesha ishara ya kwamba, kila mmoja anajidhati kwa upande wake ili kuweza kufanikisha makubaliano bora ya amani, wakati huu ambapo mazungumzo juu ya amani ya kudumu katika eneo hilo la Mashariki ya Kati yakiendelea nchini Misri.

Hata hivyo kila upande unaonekana kutofautiana kwa kiasi kikubwa katika makubaliano hayo. Israel inataka kundi la wanamgambo wa Kiislamu lenye kuidhibiti Gaza kupokonywa silaha au kuhakisha kwamba hawapati silaha kabla ya kuzingatia matakwa ya Hamas ya kuitaka Israel kuacha kuendelea kuuzingira maeneo yao hatua ambayo ilichukuliwa na Israel mwaka 2007 na baadae kuongezea nguvu na Misri.

Mvutano baina ya Israel na Hamas

Makubaliano ya pande zote mbili ya kusitisha mapigano kwa masaa 72 katika eneo hilo ilianza rasimi jioni ya jumanne, ambayo ilisaidia kuanzisha mazungumzo ya Cairo. Pande zote hizo mbili, Isreal na Hamas zipo katika shinikizo kubwa la kimataifa la kuendeleza muda wa kusitisha mapigano kwa lengo la kutoa fursa zaidi ya mazungumzo. Huku watoto nao wakionekana leo katika viwanja vya mpira vya vya shule mbalimbali

Gaza Wasserversorgung 6. August
Wapelista wakichota maji katika muda huu wa kusitishwa mapiganoPicha: MOHAMMED ABED/AFP/Getty Images

Waziri mmoja katika serikali ya Israel, Gilad Erdan, alikiambia kituo kiomoja cha radio cha Israel kwamba " Tunajitayarisha kwa hali yoyote, kama wataanzisha mashambulizi na jeshi litaanzisha pia operesheni yake"

Aliendelea kusema kimsingi Israel haipingi mabadiliko ya kiuchumi katika Gaza lakini kuondoa silaha katika eneo hilo ni muhimu. Hamas nayo imesisitiza msimamo wake kwamba muda wa kusitishwa mapigano hauwezi kuongezwa mpaka kuwe na mafanikio katika matakwa yake.

Kiongozi wa Hamas Moussa Abu Marzouk alisema mpaka jana jioni hakuna makubaliano yoyote yaliofikiwa katika usitishwaji mapigano. Izzat al-Rishq, mwanachama mwandamizi wa kundi hilo aliliambia shirika la habari la Palestina kwamba Hamas wanaweza kuongeza muda wa kuweka chini silaha kama kutatukwa na hatua iliyofikiwa katika mazungumzo yanayoendelea sasa.

Wito wa uchungzi kwenye mipaka ya Gaza

Katika hatua nyingine waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Avigdor Lieberman ametaka wakaguzi wa Umoja wa Ulaya kutupia jicho eneo la mipaka ya Gaza katika wakati huu ambapo suala la kuongezwa kwa muda wa kusitishwa mapigano ndilo linalochukua kipaumbele. Akizungumza na gazeti moja la hapa Ujerumani waziri huyo alisema isiwe polisi au wanajeshi lakini Ujerumani na Umoja wa Ulaya lazima watume wakaguzi kuangalia biashara ya Palestina na mataifa jirani.

Maafisa wa Palestina wanasema karibu watu 1,900 wameuwawa katika mapigano hayo yaliyodumu kwa takribani mwezi sasa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa robo tatu ya watu hao walikuwa raia wa kawaida. Israel inasema kiasi ya wanamgambo 900 ni miongoni mwa waliouwawa. Wanajeshi 64 wa Israel na raia watatu taifa hilo vilevile wameuwawa katika mapigano hayo yaliyoanza Julai 8 mwaka huu.

Mwandishi: Sudi Mnette/APE
Mhariri: Yusuf Saumu