1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashindano ya Riadha ya Osaka

Ramadhan Ali22 Agosti 2007

Mashindano ya riadha ya dunia yataanza jumamosi hii mjini Osaka,Japan. Msisimko utakua katika mbio na hasa majogoo wa afrika -wake kwa waume watazamiwa kutia fora.

https://p.dw.com/p/CHbD

Jumamosi hii,mashindano ya ubingwa wa riadha ulimwenguni-World Athletics Championships yatafunguliwa rasmi mjini Osaka,Japan.Wanariadha kutoka nchi 203 wanashiriki miongoni mwao wale kutoka -Kenya ,Ethiopia,Uganda na Tanzania.Idadi ya nchi zinazoshiriki mara hii imepindukia rekodi iliowekwa katika mashindano ya Seville,Spain miaka 8 iliopita.

Baada ya kuchaguliwa jana Lamine Diack,kutoka Senegal, kwa kipindi cha mwisho kama rais wa Shirikisho la riadha Ulimwenguni (IAAF),macho yanakodolewa sasa sio tu kati ya Marekani na Russia ipi itarudi na medali nyingi zaidi,bali pia kati ya dola kuu 2 za Asia:China na Japan ?

Ramadhan Ali anasimulia:

Tukianza na kuchaguliwa Lamine Diack kutoka Senegal kwa kipindi kingine cha miaka 4 kileleni mwa shirikisho la riadha la IAAF,hiki kitakuwa kipindi chake cha tatu na cha mwisho cha miaka 4.

Na hii yabainisha imani kwa uongozi wake.Msenegal huyu hakupingwa na mtetezi yeyote alipojipatia kura 167 katika mkutano was 46 wa IAAF.ni wajumbe 9 tu wsaliopiga kura kumpinga.

Diack aliparamia kileleni mwa shirikisho hilo hapo 1999 kufuatia kifo cha mtaliana Primo Nebiolo.

Pamoja na Diack wamechaguliwa huko Osaka, wanariadha maarufu kama Sebastian Coe –anaeongoza maandalio ya michezo ya olimpik ya London,2o12 itakayofuatia ya Beijing mwaka ujao.Mwengine ni bingwa wa kuruka kwa upongoo wa Ukraine,Sergey Bubka.Makamo-rais wengine ni akina Robert Hersh wa Marekani na Dahlan Al-Hamad wa Gatar.Wote watatumika kwa kipindi cha miaka 4.

Kikawaida,miaka ya nyuma kabla kusdambnaratika kwa iliokua urusi-Soviet union, dola 2 kuu zilizopimana nguvu kuparamia kilele cha orodha za medali za dhahabu,fedha na shaba ni Marekani na Urusi.

Mara hii changamoto hiyo itakuwapo,lakini kwavile mashindano haya ya ubingwa wa dunia mjini Osaka, yanatangulia yale ya Olimpik ya Beijing mwaka kamili kutoka sasa,yatatubainishia jinsi China na japan zinavyojinoa kwa kinyan’ganyiro cha mwakani.

Bara la Asia ili kujiimarisha katika medani ya riadha limekuwa karibuni likiajiri wanariadha kutoka Afrika wanaopepea bendeza za nchi za asia na sio za Afrika:

Miongoni mwa wanariadha hao ni Youssef Kamel na Rashid Ramzi wanaopepea bendera ya Bahrein.

Kenya iliwapoteza majogoo kama Wilson Kipketer aliestaafu baada ya kupepea bendera ya Denmark badala ya Kenya katika masafa ya mita 800.

Anaewaumiza kichwa wakenya ni Steven Cherono,maarufu sasa kwa jina la Saif Shaheen,anapepea bendera ya Qatar katika mita 3000 kuruka viunzi mbio ambazo Kenya inadai ni mali yake na aibu kushindwa.

Kama michezo ya olimpik,moyo wa mashindano haya msisimko utakuwa katika kutimka mbio:Katika mita 100-200 kinyan’ganyiro kitakua kati ya bingwa wa rekodi ya dunia mjamaica asafa Powel na chipukizi wapya wa Marekani.Hali itakua vivyo hivyo katika mita 400 na hii tangua wanawake hata wanaume.

Katika masafa ya kati kuanzia mita 800 hadi mbio ndefu za marathon,huo ni uwanja wa waafrika:Na hasa waethiopia wakiongozwa na Kenenisa Bekele na wakenya na wamorocco.

Kwa ufupi, mashindano haya ya Osaka ya ubingwa wa riadha yanayoanza jumamosi-August 25 na kuendelea hadi Septemba 2, yatatupa muangaza ni wanariadha gani wa kuwaangalia pale bundi zitakapolia mjini Beijing August 8,2008.Kwani huu, ni msimu unaotangulia olimpik na kila mwanariadha tangu wake kwa waume, wanajitembeza kuonesha nguvu zao na kutaka nafasi zao za kuwakilisha nchi zao katika medani ya Olimpik.

Njia ya kwenda Beijing inapitia Osaka,jumamosi hii.