1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Masilahi ya wafanyikazi na wajiri ni mamoja ulaya ?

13 Mei 2009

Umoja wa ulaya kati ya waajiri na waajiriwa.

https://p.dw.com/p/HpNy

Je, kuna kupigania masilahi tofauti kati ya Jumuiya ya waajiri katika Umoja wa Ulaya na vyama vya wafanyikazi au pande hizo mbili ni washirika ?

Ni binadamu anaestahiki kuwekwa mbele na kuhakikisha wanasiasa wana jukumu la kumtumikia.Ili kulitilia mkazo dai hili,vyama vya wafanyikahzi vimeitisha kuanzia leo hadi Jumamosi maandamano makubwa katika nchi zote za ulaya .Nini maoni ya wenye usemi juu ya mada hiyo tangu wanasiasa hata wanaviwanda ? Je, katika hali ya sasa ya msukosuko wa uchumi, masilahi ya wafanyakazi yanashughulikiwa ipasavyo ?

Ikiwa utasikiliza aliosema mjini Praghue,Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Barroso wiki iliopita wsakati wa mkutano wa kilele juu ya nafasi za kazi,basi masilahi ya wafanyikazi barani Ulaya yako kwenye mikono barabara:"Tunawaambia wananchi wetu kuwa kumpatia kila mmoja kazi ndio shabaha yetu ya kwanza.Kwani,kwa msingi wa kubomoa huduma za wanyonge,haitawezekana kuufufua uchumi."

Alisema rais wa Tume ya Umoja wa ulaya mreno Jose Barroso.

Hata rais wa wa Jumuiya ya wanaviwanda katika Umoja wa Ulaya, Bw. Ernest-Antoine Selliere, alijitokeza huko Prague kuwa mshirika mkubwa wa vyama vya wafanyikazi.

"Jitihada kubwa inafanywa na wsashirika wa misaada kwa wanyonge kuendeleza mazungumzo kati ya pande hizo mbili."

Lakini nyuma ya maneno hayo mazuri kuna kinyanganyiro cha kila upande kupigania masilahi yake .Hayo asema Bw.Reiner Hoffmann,makamo -katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyikazi la Ulaya (EGB).Akitoa mfano alitaja neno "flexicurity"-lenye maana ya mchanganyiko wa kurtegeza kamba vyama vya wafanyikazi ili nao kupatiwa usalama makazini.

Hoffmann anaongeza:

."Kimsingi, hatupingi hilo.Lakini kuregezewa kamba wanaviwanda miaka iliopita, kuliongoza kupitishwa kanuni za kuregeza vikwazo katika masoko ya kazi- mfano kuwa na uwezo wa kuwafukuza wafanyikazi kwa urahisi wakati kwa upande wapili ,usalama wa wafanyikazi kutopoteza kazi zao umepungua mno."

Kuna makundi ya watu wenye mikataba mifupi ya kazi,wafanyikazi wa kukodi ambao katika msukosuko wa sasa-asema bw.Hoffmann ndio wa kwanza kuanguka mateka.

Nchini Ufaransa n a kwengineko, kumetokea hujuma dhidi ya wakuu wa viwanda na makampuni.Wafanyikazi waliokereka wamewatekanyara kwa muda mameneja wa viwanda vyao au wameyaharibu magari yao wanayopanda.Je, hali hii yaongoza kuzuka fujo ?

Bw.Hoffmann hana uhakika iwapo msukosuko wa sasa wa kiuchumi utavinufaisha kwa muda mrefu vyama vya wafanyikazi.Mkuu wake, Katibu mkuu wa shirikisho la wafanyikazi John Monks hatahivyo, ana furahia kuona dola la ulaya linalotia maanani masilahi ya wanyonge katika jamii ghafula linawafuasi hata upande wapili wa bahari ya atlantik-anakusudia Marekani.Shirikisho la wafanyikazi la ulaya linauona msukosuko wa sasa kuwa pia ni fursa kufanikisha sera zake za kiuchumi na za kijamii.