1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yashtumiwa kwa uzalishaji wa madini ya Urani

Tatu Karema
29 Desemba 2023

Mataifa ya Magharibi yameilaani Iran kwa kuongeza uzalishaji wake wa madini ya urani iliyorutubishwa, baada ya Shirika la IAEA kusema taifa hilo limeongeza uzalishaji wake wa madini hayo

https://p.dw.com/p/4agGA
Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran  Mohammad Eslami akizungumza wakati wa mkutano  waandishi wa habari na mkuu wa IAEA Rafael Mariano Grossi  mjini Tehran mnamo Machi 4, 2023
Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran - Mohammad Eslami Picha: Vahid Salemi/AP/picture alliance

Katika taarifa ya pamoja, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Marekani zimesema ''zinalaani hatua hiyo ambayo inazidisha mpango wa nyuklia wa Iran''.

Soma pia:Iran kurutubisha madini ya Uranium kwa asilimia 20

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa ''matukio hayo ni hatua katika mwelekeo mbaya kwa upande wa Iran na kwamba maamuzi hayo yanaonesha kutokuwepo kwa dhamira kwa upande wa Iran kushiriki katika kupunguza uzalishaji huo kwa nia njema na kusababisha tabia ya kutowajibika katika mazingira ya mivutano ya kikanda.

Soma pia: Iran kurutubisha urani na kukiuka makubaliano ya nyuklia

Akijibu ripoti hiyo ya IAEA, mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran Mohammad Eslami, amesema hakuna chochote kipya walichokifanya na shughuli zao zinafuata kanuni zilizopo.