1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa yataka kurefushwa usitishwaji mapigano Gaza

Saumu Mwasimba
27 Novemba 2023

Shinikizo za kimataifa zinaongezeka zakutaka Hamas na Israel waeendelee na usitishaji vita Gaza.

https://p.dw.com/p/4ZVK1
Israel | Waziri Mkuu  Benjamin Netanyahu akitoa maelekezo kwa vikosi vya Israel
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akitoa maelekezo kwa vikosi vya IsraelPicha: Avi Ohayon/GPO/Handout via REUTERS

Shinikizo za kimataifa zimeongezeka za kulitaka kundi la Hamas na Israel kurefusha muda wa makubaliano ya kusitisha vita Ukanda wa Gaza, wakati leo ikiwa ni siku ya mwisho ya kumalizika makubaliano hayo, yaliyofunguwa njia ya kuachiwa huru kwa wafungwa na mateka.

Rais wa Marekani Joe Biden amesemausitishaji vita unapaswa kuendeleakuruhusu misaada ya kibinadamu  kuingia Gaza na kuachiliwa huru mateka zaidi wa Israel wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas.

Maafisa waaandamizi wa Umoja wa Ulaya na kutoka Jumuiya ya kujihami ya NATO pia wamepaza sauti zao kutowa mwito kama huo.

Soma pia:Rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amesema Ujerumani itasimama na Israel katika vita vyake Ukanda wa Gaza

Makubaliano ya usitishaji vita yanatarajiwa kumalizika asubuhi ya kesho Jumanne, hali ambayo inatishia kuanza upya kwa mapambano makali baada ya siku nne za utulivu.

 Chanzo kimoja kilichozungumza na shirika la habari la AFP kimesema, kundi la Hamas tayari limeonesha kuwa tayari kuendelea kusitisha vita kwa siku mbili hadi nne zaidi.