1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matatizo bado yaziandama nchi zilizokuwa katika Umoja wa Kisovieti.

Jason Nyakundi4 Mei 2009

Lengo kuu la Urusi ni kuzisambaratisha nchi hizo.

https://p.dw.com/p/HjhX
Rais wa Urusi Dmitry Medvedev.Picha: AP

Miaka minane baada ya kusambaratika Umoja wa kisovieti, mengi ya mataifa yaliyokuwemo katika umoja huo bado yanajitahidi kupata demokrasia dhabiti, huku mengi yakikabiliwa na uchumi mbaya.

Hali hii sana hutokana na udhaifu katika mifumo ya kudemokrasia, jumuiya za kiraia pamoja na sheria zinazotumiwa na chi hizi.

Urusi, kwa upande wake, lengo lake kuu ni kuyasambaratisha mataifa yaliyokuwa kwenye umoja wa kisovieti na kuyafanya kuonekana yasiyo ya maana mbele ya nchi za magharibi, na pia kuyazuia kuungana na jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi, NATO.

Serikali katika nchi hizi zimefanya kidogo sana kuimarisha uchumi wao na pia katika kujiondoa katika kuitegemea Urusi katika upande wa nishati , ajira pamoja na soko la bidhaa zake.

Ukraine, Moldova na Georgia, kwa sasa, zinapitia katika kipindi kigumu. Ukraine ambayo inapakana na Urusi, Belaruss, Moldova na Hungary zilifanikiwa kupanga mapinduzi ya mwaka 2005, lakini sasa hivi rais wa Ukraine , Victor Yushchenko, ambaye kipindi chake cha uongozi kinamalizika mwaka huu amepoteza umaarufu kabisa.

Nchini Georgia makundi ya upinzani yanaandaa maandamano kote nchini kumpinga rais Mikheil Saakashvili. Sera zake za kutaka kuijumuisha Georgia katika umoja wa Ulaya na NATO vimeshutumiwa vikali na makundi ya upinzani.

GEORGIA_SOUTH_OSSETIA_RUSSIA_MOSB115_569878122082008.jpg
Wanajeshi wa urusi wakati wa vita kati yake na Georgia.Picha: AP

Rais Saakasshvili aliyeingia madarakani kupitia kwa maandamano mitaani mwaka 2003, pia analaumiwa vikali na nchi za magharibi jinsi anavyokabiliana na makundi ya upinzani.

Umaarufu wa kiongozi huyo wa Georgia ulishuka tangu mwezi Agosti mwaka uliopita, wakati Georgia iliingia vitani na Urusi, na baada ya kushindwa kufanya mabadiliko ya kidemokrasia baada ya mapinduzi yaliyomwingiza madarakani.

Baada ya mapinduzi nchini Georgia na Ukraine, ukuaji wa demokrasia nchini Ukrain umekwama na hata kuzorota zaidi. Hata hivyo, msukosuko wa kisiasa nchini Ukrain na Gerogia umesababisha kutokuwepo uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kisiasa, hali ambayo ni tafauti nchini Moldova ambapo hali ya kisiasa imekuwa tulivu tangu utawala wa kikoministi uingie madarakani mwaka 2001, na kwa mara ya pili mwaka 2005.

Moldova ni moja ya nchi maskini zaidi barani ulaya baada ya kusambaratika Umoja wa kisoviteti mwaka 1991 huku karibu robo ya raia wa Moldova milioni nne wakifanya kazi katika nchi za umoja wa Ulaya na pia Urusi.

Huku watu wazee nchini Moldova wakiwa bado wanaitambua Urusi kama mshirika mkuu wa nchi yao, vijana wengi wanazitambua nchi za magharibi na jirani wao, Romania, ambayo lugha, tamaduni pamoja na historia vyote vinalingana na vile vya Moldova. Wengi wamekuwa wakifanya maandamano ya kuitaka Moldova ijumuishwe na Romania ambaye ni mwanachama cha Umoja nwa Ulaya na NATO:

Hata hivyo, rais Vladimir Veronin wa Moldova amekuwa akiishutumu Romania kwa kile anachokitaja kuwa inayaunga mkono maandamano yenye ghasia nchi mwake na kwa kupanga mapinduzi ya kisiasa nchini Moldova.

Maendeleo ya kidemokrasia katika mataifa yaliyokuwa katika umoja wa kisovieti hayajashindwa bali yanaingiliwa moja kwa moja na Urusi

Mwandishi : Jason Nyakundi/IPS

Mhariri : Othman Miraji