1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini ya Wakenya kupata katiba mpya yanazidi kudidimia

Josephat Nyiro Charo9 Aprili 2010

Mchakato mzima wa kuitafuta katiba hiyo unakumbwa na vikwazo. Kundi la wabunge wa mikoa ya magharibi, pwani na kaskazini mashariki wanaungana na viongozi wa makanisa kujaribu kuwashawishi wananchi kuikataa katiba mpya

https://p.dw.com/p/MsBn
Waziri mkuu Raila Odinga(kushoto) rais Mwai Kibaki (katikati) na makamu wa rais Kalonzo MusyokaPicha: AP

Ikiwa maswala nyeti kwenye katiba hiyo, yakiwemo sheria kuhusu utoaji mimba, mahakama za kadhi na sheria za kumiliki ardhi, hayatapatiwa ufumbuzi, baadhi ya wabunge nchini Kenya wanapania kuwashawishi Wakenya kupiga kura kuikataa katiba mpya iliyopendekzwa, huku kura ya maoni kuhusu katiba hiyo ikitarajiwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu.

Siku ya Alhamisi Aprili 8 mwaka huu, rais wa Kenya Mwai Kibaki, waziri mkuu Raila Odinga na makamu wa rais, Kalonzo Musyoka, walikutana na viongozi wa dini ya Kikristo kujaribu kusuluhisha mzozo uliojitokeza kuhusu kipengee kinachozungumzia utoaji mimba na mahakama za kadhi.

Viongozi wa makanisa wameapa kufanya kampeni ya kupinga vipengee hivyo ndani ya katiba hiyo havitafanyiwa marekebisho.

Josephat Charo amezungumza na Bi Jebii Kilimo, mbunge wa jimbo la Marakwet Mashariki, ambaye anaipinga katiba hiyo, na kwanza kumuuliza tatizo liko wapi.

Mtayarishaji: Josephat Charo

Mhariri: Othman Miraji