1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa nchi za nje wa Ujerumani na China wakutana Berlin

22 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cvwe

BERLIN:

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani-Frank-Walter Steinmeieer atakutana kwa mazungumzo leo mjini na cheo somo wake wa China,Yang Jiechi. Ofisi ya wizara ya mambo ya nje inasema kuwa wanamatuaini kuwa matokeo ya mkutano huo yataleta ahueni kati ya Berlin na Beijing ambao ulitiwa doa pale Kansela Angela Merkel alipokutana na Dalai lama mwezi Septemba. Kufuatia mazungumzo hao kansela alionyesha kumuunga mkono dai la Dalai Lama la Tibet kujitawala katika masuala ya kiutamaduni.China ilijibu kwa kufuta mikutano kadhaa iliokuwa ifanye na Ujerumani.