1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MECCA: Mwito wa amani kwa Washia na Wasunni wa Irak

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0e

Viongozi wa kidini wa madhehebu ya Kishia na Kisunni kutoka Irak wametia saini hati inayotoa mwito wa kuwa na amani.Hati iliyotiwa saini mjini Mecca,inasema kuwa inakatazwa kumwaga damu ya Waislamu.Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Al Arabiya,hati hiyo inayoitwa “Waraka wa Mekka” inasema,Wasunni na Washia wanapaswa kushirikiana kwa maslahi ya uhuru wa Irak na umoja wa nchi. Hati hiyo pia inatoa mwito wa kuwaachilia huru watu wasio na hatia na kuheshimu majengo yalio takatifu.Mkutano wa viongozi hao wa kidini uliofanywa nchini Saudi Arabia na kuhudhuriwa pia na waziri mkuu wa Irak Nouri al-Maliki,uliitishwa na Shirika la nchi za Kiislamu.