MELI YAZAMA,ZAIDI YA 200 WAFA
10 Septemba 2011Watu zaidi ya 200 wamekufa baada ya meli kuzama kisiwani Zanzibar.
Meli hiyo iliyokuwa inaekelea kisiwani Pemba kutokea Unguja ilikuwa na abiria zaidi ya 600.
Shirika la msalaba mwekundu limetoa taarifa hiyo. Miongoni mwa waliokufa walikuwa wanawake na watoto. Taariza zaidi zinasema kuwa watu zaidi ya 325 waliokolewa.
Sababu ya kutokea ajali hiyo haijajulikana. Lakini baadhi ya abiria wamelalamika kuwa meli iyo ilikuwa imejaa sana. Meli hiyo "MV Spice Islander" iliyokuwa imejaa sana ilizama leo alfajiri ikiwa njiani kuelekea kisiwani Pemba. Ilikuwa imejaa abiria,shehena ya mchele na bidhaa nyingine.
Rais wa Ujerumani Christian Wulff, kwa niaba ya Wajerumani wote , amemtumia Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania salamu za rambi rambi kwa msiba huo.
i