1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel ashtushwa na kifo cha balozi wa Ujerumani kwa China

6 Septemba 2021

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema ameshtushwa mno na kifo cha balozi mpya wa Ujerumani nchini China, Jan Hecker, ambaye awali alikuwa mshauri wake wa sera za kigeni.

https://p.dw.com/p/3zyHR
UK G7 2021 Cornwall | Biden, Merkel und Jan Hecker
Picha: Guido Bergmann/Bundesregierung/REUTERS

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani haijatoa sababu ya kifo cha Hecker aliyekuwa na umri wa miaka 54 na ambaye alianza kazi hiyo mwezi uliopita tu.

Naibu wake Frank Rueckert sasa ndiye atakayechukua majukumu yake. Akiwa anatokea mji wa kaskazini mwa Ujerumani wa Kiel, Hecker alikuwa wakili na aliwahi kufanya kazi kama mwanasheria na jaji.

Alikuwa na mke na watoto watatu. Kabla kuwa mshauri wa sera za kigeni wa Merkel na kuteuliwa kuwa balozi, Hecker alikuwa mhadhiri katika chuo kikuu.