1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel yaitolea wito Ulaya kupambana na ugaidi eneo la Sahel

Sekione Kitojo
2 Mei 2019

Kansela  wa  Ujerumani  Angela  Merkel  ameonya  kuhusu  hatari ya hali ya ugaidi  inayoongezeka  katika  eneo  la  Afrika  Magharibi na kuyataka  mataifa  ya  Ulaya  kuchukua  hatua dhidi  ya hali  hiyo.

https://p.dw.com/p/3HnN3
Burkina Faso Ouagadougou | Angela Merkel, Bundeskanzlerin & Treffen G5 Sahel
Picha: Reuters/A. Mimault

Kansela  Merkel  ameyasema  hayo  katika  siku  yake  ya  kwanza ya  ziara  ya  siku  tatu  katika  eneo hilo  la  Sahel, ambapo  jana aliwasili  nchini  Burkina Faso, na  pia atazitembelea  Mali  na  Niger. 

Burkina Faso Ouagadougou | Roch Marc Christian Kabore, Präsident & Angela Merkel, Bundeskanzlerin
kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kulia) akiwa pamoja na rais wa Burkina Faso Roch Marc Kabore (kushoto) mjini OuagadougouPicha: Reuters/A. Mimault

Ni  jukumu  ambalo  Ulaya  inapaswa  kuchukua , amesema  hayo jana  Jumatano  baada  ya  kukutana  na  viongozi  wa  kile kinachojulikana  kama  mataifa  ya  G5  ya  Afrika Magharibi  mjini  Ouagadougou. Iwapo hali  ya machafuko itafanikiwa katika  eneo  hili, kile tunachotaka  kukizuwia , kinaweza  kuwa katika  kiwango  kingine,"  ameonya  kansela  Merkel. Rais  wa Burkina  Faso  Roch Marc Kabore, ametaka  kuchukuliwe  hatua  za kutatua  suala  la  mzozo  wa  Libya, ambapo  amesema  vita  vya wenyewe  kwa  wenyewe  katika  nchi  hiyo  vinaathiri  eneo  lote  la Afrika  magharibi. Tatizo  hilo  ni  lazima  lipatiwe suluhisho, amesema  na  kuongeza  kwamba  bila  hivyo haitawezekana  kupiga hatua.

Ugaidi ni tatizo la kimataifa

Mapambano dhidi  ya  ugaidi  ni  suala  la  kimataifa, amesema Merkel  jana baada  ya  kukutana  na  viongozi  wa  mataifa  ya Burkina Faso, Mali, Mauritania, Niger  na  Chad  katika  mji  mkuu wa  Burkina  Faso , Ouagadougou.  Hili  sio  jukumu  la  mataifa haya  matano tu, amesisitiza Merkel , bali  ni  jukumu  pia  la  mataifa ya  Ulaya.

Burkina Faso Ouagadougou | Angela Merkel, Bundeskanzlerin & Treffen G5 Sahel
Kansela Angela Merkel (mwenye suti nyekundu katikati) akiwa katika mazungumzo na viongozi wa kile kinachoitwa G5Picha: Reuters/A. Mimault

"Marais wameeleza vizuri  kwamba  mapambano  dhidi  ya  ugaidi ni jukumu  la  kimataifa.  Ndio  sababu  naelewa matakwa  ya kuwa  na mamlaka ya  Umoja  wa  Mataifa  kwa  ajili  ya  ujumbe  wa  mataifa haya  matano ya G5 kama  ilivyofanywa  kwa  ujumbe  wa UNMISMA  lakini  kwa  mamlaka  dhabiti  zaidi."

Sekta ya maendeleo yaathirika

Sababu  ya  tahadhari  hii  ni  kutokana  na  mashambulizi yanayozidi  ya  wanamgambo  wa  Kiislamu  sio tu nchini  Mali, lakini hata  Niger na  Burkina Faso. Hali hiyo  tete  inaathiri  kwa  kiasi kikubwa  maendeleo  ya  nchi  hizi, kwa  kuwa  katika  mpaka  kati ya  Mali  na  Burkina Faso  kutokana  na  mashambulzi  haya yanayofanywa  na  wanagmabo  wa  Kiislamu  mamia  ya  shule zimelazimika  kufungwa. Bibi  Merkel  ameongeza.

"Sisi  katika  bara  la  Ulaya  tunahitaji  kuchukua  hatua  zaidi, tunahitaji  kuchukua  hatua  haraka. Baadhi  ya  mambo  tayari yameanzishwa  lakini  baadhi  bado hayajaweza  kufanyika, ndio sababu nitachukua  hatua za  dhati kuona mambo  hayo  yanatokea haraka na  yanatekelezwa haraka kwasababu  tunapaswa kuaminika na changamoto ni  kubwa."

Tatizo lingine  ni  kwamba  Marekani  inajaribu  kuzuwia  kupatikana mamlaka ya  vikosi  vya  mataifa  ya  sahel  katika  baraza  la Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa. Ujerumani itazipatia  nchi  hizo  za Sahel  kiasi  ya  euro  milioni  60  kwa  ajili  ya  jeshi  hilo  la  pamoja.

rtre, afpe