1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Messi ashinda tuzo ya Ballon d´Or

31 Oktoba 2023

Mchezaji Lionel Messi ameshinda kwa mara ya nane tuzo ya mwaka huu ya mchezaji bora wa soka duniani "Ballon d´Or". Sherehe za kutangazwa kwake zilifanyika jana usiku mjini Paris Ufaransa.

https://p.dw.com/p/4YDUA
Frankreich | 2023 Ballon d'Or in Paris | Lionel Messi
Mchezaji Lionel Messi ambaye ameshinda kwa mara ya nane tuzo ya mwaka huu ya mchezaji bora wa soka duniani "Ballon d´Or": Paris, Ufaransa: 30.10.2023Picha: Franck Fife/AFP/Getty Images

Messi mwenye umri wa miaka 36 na ambaye alishinda  tuzo ya Ballon d´Or kwa mara ya kwanza mwaka 2009, amewapiku Erling Haaland aliyechukua nafasi ya pili, Kylian Mbappe nafasi ya tatu, huku mchezaji raia wa Ubelgiji Kevin de Bruyne akishika nafasi ya nne.

Mafanikio ya Messi ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Inter Miami baada ya msimu mbaya katika timu ya Paris Saint Germain, yametokana hasa na kuiwezesha timu yake ya taifa ya Argetina kutwaa Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka jana, baada ya kuishinda Ufaransa kwa mikwaju ya penati.