1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoArgentina

Messi kujiunga na Inter Miami ya Marekani

7 Juni 2023

Mchezaji nyota wa soka duniani Lionel Messi anatazamiwa kujiunga na klabu ya kandanda ya nchini Marekani ya Inter Miami na kumaliza uvumi juu ya mpango wa kutia saini mkataba mnono wa kucheza soka nchini Saudi Arabia.

https://p.dw.com/p/4SJOj
Fussball Frankreich l Lionel Messi für Paris St. Germain l Enttäuscht
Picha: Damien Meyer/AFP

Hayo yameripotiwa hii leo na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC. 

Iwapo mkataba wake na Inter Miami utatiwa saini, itakuwa ni mara ya kwanza kwa Messi kucheza kandanda nje ya bara la Ulaya tangu alipojiunga na chuo cha kulea vipaji cha Barcelona ya Uhispania akiwa na umri wa miaka 13.

Mchezaji huyo nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, anatazamiwa pia kuikataa ofa ya kujiunga na klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kwamba Messi ambaye anaondoka kutoka klabu ya PSG ya nchini Ufaransa huenda atarejea Barcelona.

Aliondoka Barcelona mnamo mwaka 2021 baada ya kuitimikia kwa miaka 21, kutokana na sababu ya matatizo ya kifedha klabuni humo.