1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiMarekani

Mfumko wa kanda ya euro kupungua lakini kwa shakashaka

14 Aprili 2023

Mkuu wa Benki ya Ulaya Christine Lagarde amesema leo kuwa mfumuko mkubwa wa bei unaoitikisa kanda ya sarafu ya Euro utapungua ndani ya miezi michache inayokuja lakini bado kuna mashaka fulani juu ya matarajio hayo.

https://p.dw.com/p/4Q5MM
Deutschland Christine Lagarde bei der EZB-Ratssitzung mit Zinsentscheidung
Picha: Boris Roessler/dpa/picture alliance

Kupitia taarifa aliyotoa kwenye mikutano ya shirika la fedha la kimataifa - IMF inayoendelea mjini Washington, Bibi Lagarde amesema kasi ya kupanda kwa bei za bidhaa barani Ulaya itapungua ingawa mwelekeo huo unakabiliwa na changamoto.

Amesema matumaini hayo yanategemea uwezekano wa kupungua kwa bei za nishati au wasiwasi kwenye masoko ya mitaji.

Hata hivyo amesema mfumuko wa bei ambao bado umendukia wastani wa asilimia 5 hautapungua iwapo mataifa ya kanda ya Euro yataamua kupandisha mishahara ya wafanyakazi kwa kiwango kikubwa.