1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro Mashariki mwa Kongo :Hali yazidi kuwa mbaya.

6 Novemba 2008
https://p.dw.com/p/FodY
Mtoto mdogo wa kiume akimbeba nduguye wa kike katika eneo moja walikokusanyika wakimbizi kaskazini mwa mji wa Mashariki wa Goma.Picha: AP

Mapigano yanaendelea katika maeneo ya mashariki mwa Kongo kati waasi wa wanamgambo wanaoiunga mkono serikali baada ya kuzuka upya siku mbili zilizopita,licha ya waasi kutangaza hapo kabla kwamba wanasimamisha mapigano

Mapigano hayo katika mkoa wa mashariki wa Kivu Kaskazi ni kati ya waasi wanaoongozwa na Jenerali Laurent Nkunda na wanamgambo wa Mai Mai waasi hao wa Kitutsi wanaojulikana wakisemekana kuviteka vijiji vya mashariki katika mkakati wao wa kusonga mbele wakijaribu kutanua zaidi mamlaka yao katika maeneo ya mkoa huo.

Taarifa ya msemaji wa Jeshi la kimataifa la kusimamia amani nchini Kongo MONUC Luteni Kanali Jean Paul Dietrich, alidhibitisha kutekawa vijiji hivyo, akiongeza kwamba waasi wameviteka viji vya Nyanzale na Kikuku.

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa , zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kuyahama makaazi yao kwa usalama wao, tangu Nkunda alipochukua silaha 2006 kwa kile anachodai kuwalinda wale wachache wenye asili ya Kitutsi wanaujulikana huko Kongo kama Banyamulenge, dhidi ya mashambulio ya waasi wa Kihutu wa Kinyarwanda ambao wako Kongo tangu kuingia madarakani wapiganaji wa RPF baada ya mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda.

Kwa upande mwengine Jenerali Nkunda amerudia tena kitisho chake kwamba atasonga mbele hadi mji mkuu Kinshasa. Matukio haya mapya yamekuja katika wakati ambao marais wa Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yenyewe pamoja na Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa na muakilishi wa Umoja wa Afrika, wanatarajiwa kukutana katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, kuzungumzia mapigano hayo yaliosababisha janga kubwa la wakimbizi, pamoja na njia za kuusuluhisho mzozo huo.

Taarifa za kufanyika mkutano huo zilithibitishwa hapo awali na Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Kenya Moses Wetangula.Akiondoka New York jana kuelekea Nairobi, Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa alisema atakaa pamoja na Rais Joseph Kabila na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame na kusisitiza juu ya haja ya wao kusaka suluhisho la amani.

Mjini Berlin, taarifa ya wizara ya mambo ya nchi za nje wa Ujerumani ilisema waziri wa kigeni Bw Frank-Walter Steinmeier alikua na mazungumzo na rais Kagame wa Rwanda na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Kongo Alexis Tambwe Mwamba, akielezea wasi wasi wake kuhusiana na hali mashariki mwa Kongo.

Bw Steinmeier akazitaka nchi zote mbili kuhakikisha hali inaboreshwa kusaidia misaada iweze kuwafikia maelfu aya wakimbizi waliotawanyika kutokana na mapigano hayo. Wazri Steinmeier alielezea pia matumaini yake kwamba mkutano wa kesho mjini Nairobi utafungua njia ya kupatikana ufumbuzi, akiongeza kwamba matumaini ya jamii ya kimataifa yako kwenye mkutano huo.